Uchanganuzi Wakiisimu -matini wamsimuwa Tisa
View/ Open
Date
2008Author
Makanga, Miriam A
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulikia uchanganuzi wa kiisimu-matini wa diwani ya Msimu wa Tisa
kwa kujikita katika dhana za muala na mshikamano. Uchanganuzi huu umefanywa kwa
kufuata mwelekeo wa kinadharia wa muala wa Halliday na Hasan (1976) pamoja na
mwelekeo wa umatini na Beaugrande na Dressler (1981).
Utafiti huu umegawanywa katika sura nne. Katika sura ya kwanza, tumetanguliza kwa
kuelezea juu ya utanzu wa ushairi huru. Tumefafanua pia tatizo la utafiti, madhumuni ya
utafiti, na nadharia tete ambazo zimetumiwa katika utafiti huu. Sababu za kuchagua mada
hii, upeo na mipaka, na yaliyoandikwa kuhusu mada hii yanajitokeza pia katika sura hii.
Aidha, msingi na kinadharia na njia za utafiti zinakamilisha maelezo katika sura hii.
Sura ya pili imetafiti muala katika mashairi ya Msimu wa Tisa kwa kuchanganua
vipengele vya urejelezi, udondoshaji, ubadilishaji, uunganishaji na muala wa kimsamiati
na kuonyesha jinsi vinavyojenga muala. Mwishoni mwa sura hii, tumechora majedwali
yanayoonyesha vipashio mbalimbali vya muala katika mashairi ya Msimu wa Tisa.
Katika sura ya tatu, tumeanisha vipengele vya 'mshikamano kama vile: mpangilio wa
sauti, maneno, sentensi, uhusiano wa mada, anwani na yaliyomo pamoja na muktadha na
mandhari ili kubainisha namna vinavyojenga mshikamano katika mashairi ya Msimu wa
Tisa.
VI
Sura ya nne ni hitimisho na mapendekezo ambapo tumehitimisha kwa kueleza viwango
vya matumizi ya aina mbalimbali za muala. Matumizi ya vipengele vya mshikamano pia
yametolewa. Hatimaye, tumemalizia utafiti huu kwa kutoa mapendekezo ya tafiti za
kufanywa na tahakiki za baadaye.
Publisher
University of Nairobi
Subject
Uchanganuzi WakiisimuRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [606]
The following license files are associated with this item: