Show simple item record

dc.contributor.authorJanvan, Patricia W
dc.date.accessioned2024-09-17T07:09:40Z
dc.date.available2024-09-17T07:09:40Z
dc.date.issued2023
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/166583
dc.description.abstractKatika utafiti huu tumeshughulikia ukandamizaji wa jinsia ya kiume katika riwaya teule za Kiswahili: Njozi Yapata Mtenzi ya Mwenda Mbatiah (2018) na Nguu za Jadi ya Clara Momanyi (2019). Malengo ya utafiti huu ni: Kuchunguza makundi ya watu wanaokandamiza jinsia ya kiume, kubainisha athari za ukandamizaji wa jinsia ya kiume na kuchunguza mikakati ambayo wanaume wanatumia katika kupigania ukombozi wao katika riwaya teule za Kiswahili: Njozi Yapata Mtenzi (2018) na Nguu za Jadi (2019). Zaidi ya hayo, nadharia iliyotumiwa katika utafiti huu ni Nadharia ya Uwezo-Mkuu wa Kiume. Nadharia hii iliasisiwa na Connel, R. (1987) na kuendelezwa na Bly, R. (1990) na baadaye Izugbara (2005). Nadharia hii humchora mwanaume akiwa mbabe kwa misingi ya rangi nyeupe ya ngozi na ya kibayolojia, humuona mwanaume kama mtekelezaji wa majukumu yote ya familia na jamii yake kulingana na mila, itikadi na matarajio ya jamii na pia, hueleza kuwa katika jamii kuna mwanaume mpya ambaye sio mbabe nyakati zote na hana tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume. Matokeo ya utafiti huu ni pamoja na: Jinsia ya kiume imeonyeshwa kwa pande mbili. Kwanza, kuna wanaume wabinafsi ambao wanatumia ubabe wao kuwakandamiza wanaume ambao sio wababe. Pili, kuna wanaume wapya walioondokana na mfumo-dume, wanawajali wengine na wanandeleza ustawi wao, wanaume wengine na jamii yao. Utafiti huu utakuwa muhimu katika taaluma ya elimu jamii kuwahamasisha kuhusu masuala ya mahusiano mema ya kiuana na usawa wa kijinsia. Aidha, utafiti huu utakuwa muhimu katika kuendeleza taaluma ya Kiswahili hususan fasihi ya Kiswahili hasa katika uandishi wa riwaya ambao huzidi kukua na kubadilika na waandishi chipukizi wa riwaya watanufaika zaidi. Kadhalika, utafiti huu utatumika kuhamasisha jamii kuwa sio wanawake ambao hukandamizwa tu pia wanaume hukandamizwa na kuna haja ya kuangalia upya suala la ukandamizaji wa jinsia zote. Pia, utafiti wetu utatumika na watafiti wa baadaye katika kuendeleza tafiti zao.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUkandamizaji Wa Jinsia Ya Kiumeen_US
dc.titleUkandamizaji Wa Jinsia Ya Kiume Katika Riwaya Teule Za Kiswahili: Njozi Yapata Mtenzi (Mbatiah: 2018) Na Nguu Za Jadi (Momanyi: 2019)en_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States