dc.description.abstract | Katika nchi ya Kenya, wazungumzaj i hutumia lugha ya Kiingereza
ambayo ni lugha rasmi, lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya kitaifa
na lugha za kienyeji. Kwa hivyo tunaona kuwa katika nchi hii
mazingira ni ya uwingi lugha. Katika mazingira kama haya
ubadilishaji msimbo hutokea. Vile vile ubadilishaji msimbo ni jambo
ambalo hujitokeza bungeni kwa vile mazingira ya uwili lugha.
Aghalabu wabunge wengi hubadilisha msimbo kutoka lugha ya
Kiingereza hadi Kiswahili au lugha ya Kiswahili hadi Kiingereza.
Hata hivyo wakati mwingine wao hubadilisha msimbo hadi lugha za
kienyeji. Katika tasnifu hii tumezingatia ubadilishaji msimbo kutoka
lugha ya Kiswahili hadi lugha ya Kiingereza. Tumechunguza sababu
zinazowafanya wabunge kubadilisha msimbo, ni aina ipi ya
kubadilisha msimbo hujitokeza wabunge wanapobadilisha msimbo
na ni kwa kiwango kipi ambacho wao hubadilisha msimbo.
Baadhi ya sababu zinazowafanya wabunge kubadilisha msimbo ni
kama vile kutaka kutumia muda au maneno machache kueleza
j ambo fulani, kunukuu, wabunge kuwa na mielekeo hasi kuhusu
baadhi ya istilahi za Kiswahili na pia wao hubadilisha msimbo
wanapotaja majina ya mashirika na vyama vya kisiasa.
Katika utafiti huu -pia tumechunguza ama mbili za kubadilisha
msimbo ambazo hujitokeza bungeni. Aina ya kwanza ni
ubadilishaji msimbo -unaotokea baina ya sentensi na aina ya pili ni
ubadilishaji msimbo ambapo wabunge hutumia lugha zaidi ya moja
katika sentensi. Aina hii ya pili hujitokeza zaidi katika majadiliano
ya bunge.
Vile vile tumechunguza m kiwango kipi ambacho wabunge
hubadilisha msimbo.
Je, ni kwa kiwango chajuu, kadiri au kiwango cha chini. | en |