Show simple item record

dc.contributor.authorSimiyu, Jacinta N
dc.date.accessioned2012-11-13T12:33:26Z
dc.date.available2012-11-13T12:33:26Z
dc.date.issued2010
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/handle/123456789/4731
dc.description.abstractUtafiti huu unahusu kubainisha nafasi ya ulinganifu wa kipragmatiki katika tafsiri ya makala za mchezo wa kandanda magazetini. Tasnifu hii imejengwa katika msingi unaochukulia kuwa ulinganifu wa maana katika tafsiri ya makala za mchezo wa kandanda unaweza kupatikana kupitia vipengele vya kiisimu na vipengele ambavyo sio vya kiisimu, lakini zaidi kwa kuzingatia vipengele ambavyo sio vya kiisimu. Kazi za kihakiki ambazo zimewahi kufanywa katika taaluma ya tafsiri zinaegemea katika viwango vya mofolojia, semantiki na sintaksia. Katika kazi hii tunaonyesha kuwa pragmatiki ni taaluma muhimu sana inayochangia katika kupata ulinganifu wa maana kati ya matini chanzi na matini pokezi. Viwango vya mofolojia, semantiki na sintaksia ni hatua za kupata ulinganifu wa kipragmatiki. Tasnifu hii imegawanywa katika sura nne, kila moja ikijadili vipengele maalum katika suala letu la utafiti. Sura ya kwanza ina utangulizi ambao unafafanua suala letu la utafiti ambalo linahusu kubainisha nafasi ya ulinganifu wa kipragmatiki, katika viwango vya umaanisho na utaratibu wa ushirikiano na jinsi ulinganifu wa maana unavyopatikana katika tafsiri ya makala ya mchezo wa kandanda magazetini kupitia matumizi ya vipengele hivi. Aidha, tumeonyesha tatizo letu la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchagua somo, upeo na mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa, mtazamo wa kinadharia tuliotumia, njia za utafiti na hatimaye umuhimu wa utafiti. Katika sura ya pili tumeeleza mambo mbali mbali kama vile nafasi ya maana katika tafsiri na kueleza aina za maana. Tumeeleza pia ulinganifu wa kipragmatiki na jinsi ya kujenga ulinganifu wa kipragmatiki kupitia vipengele mbali mbali vya kipragmatiki vya umaanisho na utaratibu wa ushirikiano. Katika kueleza ujenzi wa ulinganifu wa kipragmatiki, tumemulika matatizo yanayoweza kujitokeza wakati wa kutafsiri vipengele hivi na kuonyesha umuhimu wa habari za kipragmatiki katika kutafsiri. Mambo haya yamefanywa kwa ajili ya kuweka msingi imara wa uchanganuzi wa makala ya mchezo wa kandanda magazetini. Sura ya tatu inahusu uchanganuzi wa makala za mchezo wa kandanda magazetini. Uchanganuzi huu umefanywa kwa kuzingatia mtazamo wa kinadharia ambao tulijadili katika sura ya kwanza. Katika uchanganuzi huu tumeonyesha jinsi vipengele vya kipragmatiki vimeshughulikiwa na kuonyesha matatizo yanayomkabili mtafsiri katika kuhamisha maana kutoka matini chanzi hadi matini pokezi. Uchunguzi wa vipengele vya kipragmatiki vya umaanisho na utaratibu wa ushirikiano umefanywa kwa kufuata mtazamo wa kinadharia wa muala. K wa kuchanganua makala za mchezo wa kandanda kwa kutumia mtazamo wa muala tumeonyesha jinsi maana iliyokusudiwa na mwandishi asilia inahamishwa kutoka matini chanzi hadi matini pokezi kwa kuzingatia vipengele vya kiisimu na vile ambavyo sio vya kiisimu. Tumebainisha kuwa ujenzi wa ulinganifu wa maana katika makala za mchezo wa kandanda unazingatia sana masuala ambayo sio ya kiisimu. Makala za mchezo wa kandanda zinazingatia sana matumizi ya vitambulishi vyote vya muala isipokuwa kitambulishi cha mahusiano ya kisarufi, ambacho ni kipengele cha kiisimu. Sura ni mahitimisho na mapendekezo ambapo tumeonyesha yale tuliyoyashughulikia, yaliyojitokeza kuhusu nadharia tete, ufaafu wa mtazamo wa tlinadharia, changamoto tulizokumbana nazo katika utafiti huu na hatimaye tukatoa mapendekezo ya utafiti mpya.en
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobi, Kenyaen
dc.titleNafasi Ya Ulinganifu Wa Kipragmatiki Katika Tafsiri Za Makala Za Mchezo Wa Kandanda Magazetinien
dc.typeThesisen


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record