• Login
    View Item 
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Science & Technology (FST)
    • View Item
    •   UoN Digital Repository Home
    • Theses and Dissertations
    • Faculty of Science & Technology (FST)
    • View Item
    JavaScript is disabled for your browser. Some features of this site may not work without it.

    Usasa Na Mwanamke Wa Kisasa Katika Nyuso Za Mwanamke Ya S.a Mohammed

    Thumbnail
    Date
    2013
    Author
    Suakei, Sivilon
    Language
    en
    Metadata
    Show full item record

    Abstract
    Malengo ya utafiti huu yalikuwa kushughulikia suala la usasa na mwanamke wa kisasa katika Nyuso za mwanamke. Hii ni riwaya yake S.A Mohammed ya mwaka wa 2010. Lengo kuu la utafiti lilikuwa kumsawiri mwanamke wa kisasa na jinsi anavyojichukua kulingana na usasa. Katika hali hiyo tuliweza kusawiri usasa na kuthibitisha kuwa Nyuso za mwanamke ni riwaya ya kisasa na tukionesha masuala makuu yanayomrejelea mhusika mkuu aliye kielelezo cha mwanamke wa kisasa. Uhusika wake unadhihirisha mambo mengi kuhusiana na usasa na vikwazo dhidi ya ufanisi wake kwa mkabala wa usasa. Aidha kuhusika kwake kunaonekana kama istiara ya mwanamke aliyetambua dhuluma zinazoendelezwa na jamii na anayepambana kupigania haki za mwanamke. Kupambana kwake ni pamoja na kuzindua jamii ili itembee na wakati. Hii ina maana ya kuasi utamaduni wenye dhana dufu zinazoirudisha jamii nyuma. Pili utendakazi wake unahusu mambo mengi na makubwa ambayo jamii huona vigumu kutekelezwa na mwanamke. Nadharia iliyotuongoza katika utafiti huu ni ya ufeministi wa kiafrika. Ilitufaa maana inayo miongozo iliyotuelekeza kujua ni yapi mwanamke wa kiafrika hupitia na anavyojitahidi kujinasua kutoka kwa dhuluma hizo. Ili kujipa ufahamu zaidi tuliweza kudurusu tasnifu zilizoshughulikiwa na ambazo zilihusiana na suala letu. Tasnifu hizo zilisawiri maonevu dhidi ya mwanamke wa kiafrika lakini hazikuangazia ni jinsi gani mwanamke wa kisasa anavyokabiliana na dhuluma kama hizo na zinazoendelezwa hata katika jamii ya sasa. Kuweza kutekeleza wajibu wa utafiti, tumegawa tasnifu hii katika sura tano. Sura ya kwanza ni kuhusu uteuzi wa mada, madhumuni, msingi wa nadharia na njia za utafiti. Sura ya pili inayo mukhtasari wa riwaya ya utafiti na vilevile imeshughulikia dhana muhimu ambazo zimehalalisha usasa unaojitokeza katika riwaya yetu ya utafiti. Sura ya tatu inarejelea maudhui yanayojikita kwenye utamaduni na yanayokinzana na usasa. Aidha inaonesha utendakazi ambao unadhibitisha kuwa mhusika mkuu ni mwanamke wa kisasa na aliyeajibika kulingana na usasa. Sura ya nne imesawiri ithibati kadhaa zinazoonesha kufaulu kwa mwanamke wa kisasa na masuala ibuka yanayokwaza ufanisi wake. Kufikia mwisho wa sura hii tunarejelea mikakati iliyofanikisha ndoto zake na alivyozifuatilia kama suala la kimsingi la kufanikisha utendakazi wake. Sura ya tano ni ujumla wa matokeo ya yaliyoshughulikiwa na mapendekezo ya yale yanayoweza kutafitiwa kwa kina ili kukamilisha kwa dhati suala hilo tulilolishughulikia
    URI
    http://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/59457
    Publisher
    University of Nairobi
    Collections
    • Faculty of Science & Technology (FST) [3799]

    Copyright © 2019 
    University of Nairobi Library
    | UoN Quality Policy | Send Feedback
     

    Browse

    All of UoN Digital RepositoryCommunities & CollectionsBy Issue DateAuthorsTitlesSubjectsThis CollectionBy Issue DateAuthorsTitlesSubjects

    My Account

    LoginRegister

    Copyright © 2019 
    University of Nairobi Library
    | UoN Quality Policy | Send Feedback