Show simple item record

dc.contributor.authorSuakei, Sivilon
dc.date.accessioned2013-11-19T09:27:51Z
dc.date.available2013-11-19T09:27:51Z
dc.date.issued2013
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/59457
dc.description.abstractMalengo ya utafiti huu yalikuwa kushughulikia suala la usasa na mwanamke wa kisasa katika Nyuso za mwanamke. Hii ni riwaya yake S.A Mohammed ya mwaka wa 2010. Lengo kuu la utafiti lilikuwa kumsawiri mwanamke wa kisasa na jinsi anavyojichukua kulingana na usasa. Katika hali hiyo tuliweza kusawiri usasa na kuthibitisha kuwa Nyuso za mwanamke ni riwaya ya kisasa na tukionesha masuala makuu yanayomrejelea mhusika mkuu aliye kielelezo cha mwanamke wa kisasa. Uhusika wake unadhihirisha mambo mengi kuhusiana na usasa na vikwazo dhidi ya ufanisi wake kwa mkabala wa usasa. Aidha kuhusika kwake kunaonekana kama istiara ya mwanamke aliyetambua dhuluma zinazoendelezwa na jamii na anayepambana kupigania haki za mwanamke. Kupambana kwake ni pamoja na kuzindua jamii ili itembee na wakati. Hii ina maana ya kuasi utamaduni wenye dhana dufu zinazoirudisha jamii nyuma. Pili utendakazi wake unahusu mambo mengi na makubwa ambayo jamii huona vigumu kutekelezwa na mwanamke. Nadharia iliyotuongoza katika utafiti huu ni ya ufeministi wa kiafrika. Ilitufaa maana inayo miongozo iliyotuelekeza kujua ni yapi mwanamke wa kiafrika hupitia na anavyojitahidi kujinasua kutoka kwa dhuluma hizo. Ili kujipa ufahamu zaidi tuliweza kudurusu tasnifu zilizoshughulikiwa na ambazo zilihusiana na suala letu. Tasnifu hizo zilisawiri maonevu dhidi ya mwanamke wa kiafrika lakini hazikuangazia ni jinsi gani mwanamke wa kisasa anavyokabiliana na dhuluma kama hizo na zinazoendelezwa hata katika jamii ya sasa. Kuweza kutekeleza wajibu wa utafiti, tumegawa tasnifu hii katika sura tano. Sura ya kwanza ni kuhusu uteuzi wa mada, madhumuni, msingi wa nadharia na njia za utafiti. Sura ya pili inayo mukhtasari wa riwaya ya utafiti na vilevile imeshughulikia dhana muhimu ambazo zimehalalisha usasa unaojitokeza katika riwaya yetu ya utafiti. Sura ya tatu inarejelea maudhui yanayojikita kwenye utamaduni na yanayokinzana na usasa. Aidha inaonesha utendakazi ambao unadhibitisha kuwa mhusika mkuu ni mwanamke wa kisasa na aliyeajibika kulingana na usasa. Sura ya nne imesawiri ithibati kadhaa zinazoonesha kufaulu kwa mwanamke wa kisasa na masuala ibuka yanayokwaza ufanisi wake. Kufikia mwisho wa sura hii tunarejelea mikakati iliyofanikisha ndoto zake na alivyozifuatilia kama suala la kimsingi la kufanikisha utendakazi wake. Sura ya tano ni ujumla wa matokeo ya yaliyoshughulikiwa na mapendekezo ya yale yanayoweza kutafitiwa kwa kina ili kukamilisha kwa dhati suala hilo tulilolishughulikiaen
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleUsasa Na Mwanamke Wa Kisasa Katika Nyuso Za Mwanamke Ya S.a Mohammeden


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record