Uchanganuzi wa makosa yanayofanywa na wanafunzi wazungumzaji wa lugha ya Ekegusii
Abstract
Madhumuni ya utafiti huu ni kuchanganua makosa ya kifonolojia, kimofolojia na kisintaksia
yanayojitokeza katika kazi za Kiswahili zilizoandikwa na wanafunzi wazungumzaji wa lugha
ya Ekegusii. Utafiti huu ulitathmini ni kwa kiwango kipi lugha ya Ekegusii inachangia
makosa hayo. Ili kufikia malengo ya utafiti huu, wanafunzi kutoka viwango viwili tofauti vya
usomi waliandika insha ambazo zilisahihishwa na makosa yaliyopatikana kuchanganuliwa
kwa misingi ya mtazamo wa Uchanganuzi Makosa. Makosa hayo yaliainishwa katika
kategoria mbalimbali kisha sababu zinazosababisha makosa hayo kuelezwa. Matokeo ya
utafiti huu yalionyesha kuwepo kwa makosa haya katika viwango vyote japo kadiri
mwanafunzi anavyoendelea na masomo katika viwango vya juu, makosa yanapungua. Lugha
ya Ekegusii ilichangia pakubwa kutokea kwa makosa haya.
Citation
Shahada ya uzamili ya KiswahiliPublisher
University of Nairobi