Ukiukaji Wa Kanuni Za Upole Katika Mhanga Nafsi Yangu
Abstract
Upole ni suala muhimu sana katika kuanzisha na kudumisha mahusiano mema baina ya wanajamii. Ili kudumisha mahusiano hayo, wazungumzaji wakati wote hulazimika kutumia mikakati mbalimbali ya upole ili kuhifadhi nyuso zao na za wenzao.Tasnifu hii ni uchunguzi wa jinsi ukiushi wa kanuni za upole umetumiwa katika Mhanga Nafsi Yangu ili kujenga na kuendeleza maudhui. Uchunguzi huu ulinuia kubainisha iwapo ukiushi wa kanuni za upole katika riwaya hii umefaulu kujenga na kuendeleza maudhui makuu katika riwaya teule. Ulinuia pia kubainisha ni wahusika wapi wametumiwa kuendeleza maudhui makuu. Tulikusudia pia kuchunguza kama nadharia ya upole ya Brown na Levinson (1987, 1978) na kanuni za upole za Grice (1975) zinaweza kutumika kuchanganua kazi ya fasihi andishi
Publisher
University of Nairobi