Sajili Ya Matangazo Ya Biashara: Mtazamo Wa Kipragmatiki
Abstract
Lengo kuu la utafiti huu ni kuchanganua lugha katika sajili ya biashara kwa kutumia
mtazamo wa Kipragmatiki. Tumeangazia lugha kimaandishi na kimazungumzo. Kazi hii
imegawika katika sehemu tano. Sura ya kwanza imetanguliza kazi yote kwa kuangazia
mada ya utafiti. Sura ya tano imetoa muhtasari wa kazi yote. Nadharia tete zifuatazo
zimeongoza utafiti huu; maswala yanayoathiri matumizi ya lugha ya matangazo ya
biashara ni hadhira inayolengwa na washindani ya kibiashara, lugha inayotumiwa katika
matangazo ya biashara hukiuka kaida za mfumo wa lugha kwa lengo la kumnufaisha
mtoaji wa matangazo ya biashara, lugha zungumzwa huwa na athari kubwa kutokana na
uchochezi wake wa kiakili kuliko lugha andishi kwenye matangazo ya biashara.
Uchunguzi wetu tumeufanya kwa kufuata muongozo wa nadharia tatu. Nadharia ya
kwanza ni nadharia ya uhusiano iliyoasisiwa na Wilson, D. na Sperber, D. (2004).
Nadharia hii imetuongoza kuchunguza ujumbe unaowasilishwa katika matangazo ya
biashara na uhusika wa mlengwa katika ujumbe huo. Nadharia ya pili ambayo tumetumia
ni ya umaanisho ambayo iliasisiwa na Grice, H.P (1975). Nadharia hii imetuongoza
kuchunguza maana katika matangazo ya biashara, huku tukizingatia maana wazi na
maana fiche/ ya umaanisho katika matangazo husika. Nadharia ya tatu ni ya vitendo
usemi iliyoasisiwa na Justin, J. L (1962). Nadharia hii imetuwezesha kuchunguza
utendaji wa lugha katika matangazo ya biashara. Nadharia hizi tatu tumezutumia kwa
ushikirikiano yaani zote kwa pamoja. Data yetu kimaandishi tumeipata kutoka kwa jarida
la Kilimo Bora, Gazeti la Taifa Leo, matangazo ya biashara kutoka kwa Wizara ya Afya
na kwenye mabango. Data kimazungumzo tumeikusanya kutoka soko kuu la vyakula la
Thika. Matokeo ya utafiti wetu yamebainisha kuwa lugha katika matangazo ya biashara
hutumiwa na mtangazaji kimaksudi ili kumvutia mlengwa. Ushawishi na uchochezi wa
kiakili katika lugha ya matangazo ya biashara hufanikisha uwasilishaji na upokezi wa
matangazo haya.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: