Mtindo Katika Utenzi Wa Katirifu.
View/ Open
Date
2016Author
Nyamari Roseline K
Type
ThesisLanguage
enMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu umehusu namna ambavyo mtindo umetumika katika Utenzi wa Katirifu
mswada wa Knappert (1979). Tumehakiki vipengele vya kimtindo ambavyo ni
wahusika, taswira, dayalojia na tamathali nyingine za usemi zikiwemo maswali ya
balagha, tashihisi, tashibihi, chuku na sitiari. Katika kuhakiki hayo, tumeitumia
nadharia ya Umitindo. Tumeongozwa na malengo mawili ya utafiti. Kwanza,
kuhakiki vipengele vya kimtindo katika Utenzi wa Katirifuna pili, kubainisha
umuhimu wa vipengele hivyo katika kuwasilisha dhamira na maudhui ya mtunzi.
Kuhusu wahusika, tumehakiki sifa zinazowatambulisha na uhusika wao katika Utenzi
wa Katirifu. Wahusika wasaidizi wamewasaidia wahusika wakuu katika kujenga na
kukamilisha maudhui ya mwandishi. Taswira, dayalojia na tamathali za usemi
zimetumiwa kuwasilisha dhamira na maudhui yake. Kuna mandhari ya kijiografia na
yale ya kinjozi. Maswali yetu ya utafiti yamepata kujibiwa kikamilifu kwa kuwa
tumeweza kubaini vipengele vya kimtindo na pia kuonyesha umuhimu wa vipengele
hivyo katika uwasilishaji wa dhamira na maudhui. Hatahivyo, kuna changamoto
tulizozipitia. Hatimaye, tumetoa mapendekezo kwa watakaofanya tafiti za baadaye
kuhusiana na Utenzi wa Katirifu.
Publisher
University Of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: