Uwasilishaji Wa Ufeministi Kinzani Katika Kiswahili Kupitia Tafsiri: Tathmini Ya Riwaya Ya Barua Ndefu Kama Hii
![Thumbnail](/bitstream/handle/11295/100203/Yegon_Uwasilishaji%20Wa%20Ufeministi%20Kinzani%20Katika%20Kiswahili%20Kupitia%20Tafsiri%20Tathmini%20Ya%20Riwaya%20Ya%20Barua%20Ndefu%20Kama%20Hii.pdf.jpg?sequence=6&isAllowed=y)
View/ Open
Date
2016Author
Yegon, Magdaline C
Type
ThesisLanguage
OthersMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulikia uwasilishaji wa ufeministi kinzani katika Kiswahili kupitia tafsiri kwa kujikita katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii. Tulilenga kuchunguza uelewa unaoibuliwa na masuala ya ufeministi katika Kiswahili na kuchunguza namna ufeministi kinzani unajibainisha katika riwaya ya Barua Ndefu Kama Hii kasha kuhitimisha kwamba ufeministi kinzani unafikishwa hadi fasihi ya Kiswahili kupitia Kiswahili. Kwa kuegemea nadharia ya ufeministi wa Kiafrika na ya ulinganifu amilifu tulichunguza masuala ya ufeministi yaliyoibua ufeministi kinzani kama; usasa na ukale wa ndoa, usasa na ukale wa elimu, usasa, mahusiko ya wanandoa katika ulezi, changamoto za kuacha desturi na kukumbatia elimu na usasa na nafasi za uongozi, na kuchunguza mahusiano ya wahusika riwayani ambayo yanasababisha majukumu na misimamo inayokinzana ya wanawake kuhusu masuala ya kifeministi kama; mahusiano baina ya Aisatu na Ramatulayi kwa upande mmoja na Binetuu, Bibi Mama- mkwe na Shangazi Nabu kwa upande ule mwingine. Matokeo yetu yalidhihirisha kuwa upo uelewa kinzani wa masuala ya kifeministi katika fasihi ya Kiswahili. Ufeministi huu kinzani hujitokeza katika mawasilisho kinzani ya masuala ya kifeministi na mawasilisho ya mitazamo kinzani ya wanawake kuhusu masuala ya kifeministi katika riwaya. Hatimaye tumeweza kuhitimisha kwamba maudhui haya ya ufeministi kinzani yamefikishwa katika fasihi ya Kiswahili kupitia tafsiri.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: