Show simple item record

dc.contributor.authorMakena, Mwenda Elizabeth
dc.date.accessioned2019-01-24T12:34:05Z
dc.date.available2019-01-24T12:34:05Z
dc.date.issued2018
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/105468
dc.description.abstractKazi yetu imechunguza jinsi baadhi ya vipengele vya fani: mandhari, wahusika na mianzo na vimalizio vinavyochangiana na kukamilishana ili kuwasilisha maudhui katika hadithi fupi za Said A. Mohamed. Fani ni jinsi ambavyo msanii hufinyanga kazi yake ili msomaji apate ujumbe wake kwa njia iliyo nzuri. Kazi yetu imetumia Nadharia ya Umuundo kuchambua vipengele vya fani. Tumechunguza jinsi mwandishi ametumia mandhari katika kufanikisha uwasilishaji wa maudhui. Pia tumetathmini nafasi ya wahusika wakuu na wadogo katika kufanikisha uwasilishaji wa maudhui. Aidha, tumeangazia jinsi mwandishi alivyotumia mianzo na vimalizio vya hadithi fupi katika kufanikisha uwasilishaji wa maudhui. Kutokana na uchunguzi huu, imebainika kuwa mwandishi ametumia vipengele vya fani kukuza maudhui kwa ufundi mkubwa sana. Vipengele vyenyewe ni kama vile mandhari tofautitofauti yaliyofanikisha uwasilishaji wa maudhui. Mwandishi ametumia wahusika kiufundi katika kuupitisha ujumbe wake. Usawari wa wahusika umefanywa kiufundi ili kuafiki matarajio ya hadithi fupi.Hatimaye tumeshughulikia kipengele cha msuko na kudhibitisha kwamba msuko wa hadithi fupi huwa sahili. Tumemulika msuko wa hadithi fupi hasa kwa kuangazia uanzaji na utamatishaji wa hadithi husika. Mwandishi wa hadithi fupi zilizoteuliwa amedhihirisha ya kwamba vipengele vya fani: mandhari, wahusika na mianzo na vimalizio vya hadithi fupi vinachangiana na kukamilishana ili kufanikisha uwasilishaji wa maudhui. Tumegundua ya kwamba nadharia ya Umuundo imefaa kazi hii kwa sababu tumeona ya kwamba nadharia hii inaangazia vipengele vya kazi ya sanaa jinsi vinavyohusiana na kujengana.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUwasilishaji Wa Maudhui Katika Hadithi Fupi Teule Za Said A. Mohameden_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States