Show simple item record

dc.contributor.authorMakanji, Nicholus N
dc.date.accessioned2020-02-27T07:04:04Z
dc.date.available2020-02-27T07:04:04Z
dc.date.issued2019
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/108616
dc.description.abstractKazi hii ilihusu uhawilishaji wa fonimu za Kikisa katika lugha ya Kiswahili Sanifu. Kazi hii ilihusisha ubainishaji wa makosa katika insha za wanafunzi na tathmini ya athari za makosa hayo katika uelewekaji wa maana katika Kiswahili Sanifu. Utafiti huu ulitumia lugha ya Kikisa kama lugha ya kwanza na lugha ya Kiswahili Sanifu kama lugha ya pili. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Makosa na Lugha Kati kubainisha athari za Kikisa zijitokezazo katika Kiswahili Sanifu wakati wazungumzaji asilia wa Kikisa wanapotumia Kiswahili Sanifu. Mbinu za usomaji matini, utumiaji wa hojaji, uchunguzi shiriki na mahojiano zilitumika katika ukusanyaji data huku mbinu za uchanganuzi wa data zikitumika kwa kuongozwa na nadharia ya Uchanganuzi Makosa na Lugha Kati. Kazi hii ilitathmini athari za uhawilishaji wa fonimu za Kikisa katika Kiswahili kwa maana ya usemi na maandishi ya mzungumzaji na mwandishi aliye mzungumzaji asilia wa Kikisa. Athari za uhawilishaji huu wa fonimu kwa maana zilichunguzwa katika kazi hii ili kutathmini uwezo wa uhawilishaji fonimu kimakosa katika kufanikisha au kutofanikisha mawasiliano baina ya mzungumzaji mahiri wa Kiswahili Sanifu na mzungumzaji wa Kiswahili aliye mzungumzaji asilia wa Kikisa. Hili limefikiwa kupitia kubainisha tofauti za maana zinazojitokeza fonimu inapobadilishwa kutokana na uhawilishaji mbaya wa fonimu za Kikisa katika Kiswahili Sanifu. Malengo ya utafiti huu yalikuwa kuonyesha tofauti za kifonimu baina ya Kikisa na Kiswahili na kutathmini athari za tofauti hizi kwa matamshi na maana zijitokezazo katika Kiswahili Sanifu. Matokeo ya utafiti huu yalibainisha hali tatu za uelewekaji wa makosa ambao ulikuwa na athari tofauti kwa mawasiliano baina ya mzungumzaji wa Kiswahili aliye mzungumzaji asilia wa Kikisa na msikilizaji mahiri wa Kiswahili Sanifu. Kazi hii ilibainisha makosa yanayosababisha athari zisizoathiri maana, zinazobadili maana na zinazopoteza maana husika kabisa. Athari zinazobadili maana na zinazopoteza maana zilitokea kuwa na athari kubwa kwa mawasiliano.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity Of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectAthari Za Uhawilishajien_US
dc.titleAthari Za Uhawilishaji Wa Vitamkwa Vya Kikisa Katika Maana Zijitokezazo Katika Kiswahili Sanifuen_US
dc.typeThesisen_US
dc.contributor.supervisorMukhwana, Ayub
dc.contributor.supervisorIribe, Mwangi


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States