Muundo Na Uamilifu Wa Chagizo Katika Virai Na Vishazi Vya Kiswahili Sanifu
Abstract
Mada yetu ya utafiti ilikuwa uamilifu wa chagizo katika virai na vishazi vya Kiswahili sanifu.Tulidhamiria kuchunguza viambajengo vya aina tofauti za chagizo katika virai na vishazi vya Kiswahili sanifu huku tukilenga kuonyesha miundo tofauti inayowakilishwa na aina hizi za chagizo. Tulikusudia kubaini iwapo chagizo zenye miundo fulani huwakilisha majukumu yale yale ya theta au tofauti iwapo nafasi ya chagizo husika itabadilishwa katika sentensi fulani. Utafiti wetu ulitumia nadharia ya X-baa na Theta. Nadharia ya X-baa ilitumika kubainisha miundo tofauti inayowakilishwa na chagizo katika virai na vishazi vya Kiswahili sanifu na ile ya Theta ilitumiwa kutambua majukumu tofauti ya theta yanayowakilishwa na chagizo hizi katika virai na vishazi vya Kiswahili sanifu.Data iliyotumika katika utafiti wetu ilidondolewa kutoka kwa vitabu vitatu tofauti ambavyo vilihusisha sentensi zilizokuwa na kipashio chagizo ambazo zilidondolewa na kuchanganuliwa kwa misingi ya nadharia tofauti. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo na kupitia kwa vielelezo tungo.Ilibainika kuwa kipashio chagizo ambacho ni cha ziada katika virai na vishazi vya Kiswahili sanifu huwa na miundo tofauti iliyoundwa kwa viambajengo tofauti na kwamba chagizo hizi huwakilisha majukumu tofauti ya theta kutegemea kinafafanua kirai kipi katika sentensi. Vilevile ilikuwa wazi kuwa chagizo zilizo na muundo sawia zaweza kuwakilisha majukumu tofauti ya theta kulingana na kitenzi kinachotoa jukumu hili la theta kwacho.
Publisher
University of Nairobi
Subject
Virai Na VishaziRights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: