Show simple item record

dc.contributor.authorWafula, Michael
dc.date.accessioned2020-05-20T06:51:48Z
dc.date.available2020-05-20T06:51:48Z
dc.date.issued2019
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/109692
dc.description.abstractUtafiti huu unalenga kubainisha namna mtazamo wa kipragmatiki unaweza kutumiwa kuihakiki kazi ya fasihi. Ili kufanikisha lengo hili, tamthilia ya Pango iliteuliwa kimakusudi ili ilitupatie data ya utafiti huu. Data ya utafiti huu ilitokana na uchunguzi wa kauli za wahusika mbalimbali katika tamthilia teule na kuzichanganua kwa msingi wa Nadharia ya Utoupole ya Culpeper (1996). Lengo la kwanza la utafiti huu lilikuwa kubainisha mikakati ya utoupole ambayo inatumiwa na wahusika wanapoingiliana na wenzao ili kufanikisha mazungumzo yao. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa wahusika katika tamthilia ya Pango wanatumia mikakati ya utoupole ili kudhuru nyuso za wenzao ili kudhoofisha au kuvunja mawasiliano miongoni mwao. Lengo la pili la utafiti huu lilikuwa kubainisha namna mikakati ya utoupole inayotumiwa na wahusika katika tamthilia ya Pango inachangia katika ukuzaji wa sifa zao. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa sifa za wahusika mbalimbali zikiwa ni pamoja na hasi na chanya zimebainika kupitia matumizi yao ya mikakati ya utoupole. Vilevile, utafiti huu ulilenga kubainisha namna mikakati ya utoupole inayotumiwa na wahusika inaendeleza maudhui katika tamthilia ya Pango. Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha kuwa mikakati ya utoupole inayotumiwa na wahusika mbalimbali inaendeleza maudhui mbalimbali.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectTamthilia Ya Pangoen_US
dc.titleMikakati Ya Utoupole Katika Tamthilia Ya Pango Ya Kyallo Wadi Wamitilaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States