Show simple item record

dc.contributor.authorMuteti, Agnes M
dc.date.accessioned2021-01-19T08:37:17Z
dc.date.available2021-01-19T08:37:17Z
dc.date.issued2020
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/153653
dc.description.abstractUtafiti huu unashughulikia upole na utoupole katika Pendo la Karaha. Riwaya hii iliteuliwa kimakusudi ili kupata data iliyoweza kufanikisha malengo ya utafiti huu. Data ya kimsingi ya utafiti ilitokana na uchanganuzi wa kauli mbalimbali za wahusika. Kauli za wahusika zilichanganuliwa katika misingi ya nadharia mbili za kipragmatiki. Kila nadharia ilikuwa na wajibu wake tofauti katika kazi hii. Nadharia ya Upole iliyopendekezwa na Brown na Levinson (1987) ilikuwa na wajibu wa kuchunguza upole katika riwaya yote. Nadharia ya Utoupole iliyopendekezwa na Culpeper (1996) nayo ilitekeleza wajibu wa kuchunguza kuwepo kwa utoupole katika Pendo la Karaha. Lengo la kwanza la utafiti huu lilihusu kuchunguza upole katika riwaya teule. Ilibainika kuwa mikakati ya upole iliyopendekezwa na Brown na Levinson ilidhihirika kikamilifu katika riwaya teule. Lengo la pili la utafiti huu lilikuwa kubaini utoupole katika Pendo la Karaha. Ilibainika kuwa mikakati ya utoupole iliyopendekezwa na Culpeper (1996) ilidhihirika kikamilifu katika riwaya teule. Lengo la tatu lililohusu kubainisha matendo yanayoathiri nyuso za wahusika liliafikiwa vilevile. Ilibainika kuwa matendo yaliyoathiri zaidi nyuso hasi za wasikilizaji katika Pendo la Karaha yalijumuisha matendo ya msikilizaji kuarifu kuhusu vitendo hasi vijavyo, matendo ya msemaji yaliyoarifu msikilizaji kitendo kilichotarajiwa kuwepo na matendo yaliyoarifu matamanio ya msemaji kwa msikilizaji. Matendo yaliyoathiri nyuso chanya za wasikilizaji yalibainika kupitia matendo yaliyodhihirisha maoni hasi ya msemaji kuhusu uso chanya wa msikilizaji na msemaji kumpuuza msikilizajien_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUpole Na Utoupole Katika Pendo La Karahaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States