Show simple item record

dc.contributor.authorMburu, Peter N
dc.date.accessioned2021-08-20T08:07:24Z
dc.date.available2021-08-20T08:07:24Z
dc.date.issued2011
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155293
dc.description.abstractTasnifu hii inahusu jumbe zinazopatikana katika magari ya usafiri wa umma yanayojulikana kama Matatu. Utafiti wetu umefanyiwa mjini Nyahururu ambao ni mji unaopatikana katika jimbo la Nyandarua, takribani kilomita mia moja themanini kaskazini mwa jiji kuu la Kenya, Nairobi. Utafiti huu umegawanywa katika sura tano. Katika sura ya kwanza, tumelenga kutanguliza mada, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti na nadharia tete zitakazotuongoza katika utafiti wetu. Aidha tumeziangalia sababu zetu za kuchagua mada pamoja na upeo na mipaka ya uchunguzi wetu, yaliyoandikwa kuhusu mada yetu, msingi wa nadharia na hatimaye mbinu zilizotumika katika utafiti huu. Sura ya pili imelenga kuchunguza mitindo iliyotumiwa katika maandishi ya vibandiko. Sura ya tatu imeshughulikia matumizi ya sentensi na tamathali za userni pamwe na jumbe katika matatu. Katika sura ya nne, tumechunguza hisia na maoni ya wasafiri na waandishi wa jumbe zenyewe kuhusu jumbe kwenye magari ya matatu. Katika sura ya tano, tumetathmini matokeo ya uchunguzi wetu, na pia kutoa mahitimisho na mapendekezo ya utafiti wa baadaye.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisheruniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectJumbe , Vibandiko vya Matatuen_US
dc.titleJumbe katika Vibandiko vya Matatuen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States