dc.description.abstract | Tasnifu hii imeshughulikia uchambuzi wa maudhui makuu katika Utenzi wa
Abdirrahmani na Sufiyani kwa kusoma utenzi wenyewe na kudondoa yale masuala
mazito yenye uyakinifu katika maisha ya jamii. Tumeongozwa na nadharia ya
uyakinifu wa kijamii katika kuchanganua maudhui haya makuu yaliyojitokeza wazi
katika jamii ya jadi na pia katika jamii ya sasa. Maudhui haya ni kama vile dini,
usaliti na dhuluma, ndoa na mapenzi, ushujaa, vita na maridhiano. Tuliweza
kuoanisha masuala haya na nadharia ya uyakinifu wa kijamii kwani kulingana na
mihimili yake, masuala yanayoelezwa katika utenzi wetu, yanazingatia hali halisi
yanayoikumba jamii katika vigezo vitatu: kisosholojia, kiuchumi na kisiasa. Vilevile
jamii hutathmini maendeleo yake kutokana na vigezo hivi ili iweze kupiga hatua.
Tuliweza kusoma kazi mbalimbali zinazohusiana na utenzi ili kupata mwelekeo mzuri
wa kutusaidia kufanya uchambuzi wa maudhui makuu katika Utenzi wa
Abdirrahmani na Sufiyani kama kazi yetu husika. Tumewasilisha masuala
tuliyoyachanganua kupitia maelezo na ufafanuzi mwafaka kwa kuonyesha jinsi
maudhui haya yanavyoweza kuleta matokeo hasi na chanya katika jamii ya sasa.
Kutokana na utathmini wetu, tumedhihirisha wazi kwamba dini ndilo suala kuu
linalozaa masuala au maudhui mengine tuliyoyachambua kama vile usaliti na
dhuluma, ndoa na mapenzi, ushujaa, vita na maridhiano. Mtagusano wa wanajamii
huleta tofauti mbalimbali katika jamii kwa mfano tofauti za kidini huleta vita, usaliti
na dhuluma miongoni mwao. Vilevile utangamano mzuri hufanya jamii kuishi katika
ndoa iliyo na mapenzi na ambayo hujenga uhusiano mwema katika jamii kupitia dini. | en_US |