Ukiushi Katika Lugha Ya Kimaongezi Dhidi Yakanuni Za Kiswahili Sanifu
Abstract
Utafiti huu umetokana na imani ~wa~ba ukiushi katika
lugha ya kireaongezi ni tukio halisi na dhahiri katika
matumizi ya lugha yo yote ile. (Taz. Max Black, 1968).
Kuifahamu lugha na kuielewa kikamilifu kunahusu pia ufahamu
wa hali ya ukiushi na sababu za ukiushi huo unaotokea.
Tasnifu hii imechunguza na kuonyesha baadhi ya makosa
(ukiushi) yanayotokea katika hali halisi ya maongezi ya
wahusika kutoka katika mtaa wa Kariobangi South, wjini
Nairobi.
Kazi hii imegawanywa katika sura sita. Kila sura
inajadili kipengee maalum kinachohusu matumizi ya lugha.
Kila sura ina utangulizi, na panapo hitajika, kiishio
kinachotoa muhtasari na uamuzi wa jumla kulingana na
matokeo ya utafiti.
Sura ya kwanza ni sura hii unatoa utangulizi wa utafiti. Utangulizi
wa maelezo machache kuhusu mtaa wa Kariobangi South (tulikofanyia utafiti) na wakazi ~Jake.
Katika sura hii pia tumejadili somo letu la utafiti,
madhumuni yetu ya kuufanya utafiti huu na upeo wa tasnifu.
Zaidi ya hayo pia tumeelezea kuhusu nadharia tunayoitumia
kama kigezo cha kupimia matumizi ya lugha. Katika sehemu
ya 'Yaliyofanywa kuhusu somo', tunajadili baadhi ya kazi
zingine zilizofanywa na kuandikwa na ~mbazo, kwa namna
fulani, zinahusiana na utafiti wetu. Tunatoa sababu zetu
za kulichagua so~o katika sura hiyo ya kwanza. Fauka ya
hayo, tunatoa maelezo kuhusu haipothesia zinazopimwa katika
utafiti huu na njia tulizozitumia katika kuufanya utafiti
wetu. Sura ya pili inayashughulikia masiala muhimu kuhusu
lugha ya Kiswahili na matumizi yake kwa jumla.
Tunaziangalia hoja za usanifishaji wa lugha na dhana ya
ukiushi katika matumizi ya lugha; na kuelezea jinsi ambavyo
ukiushi unadhihirika kulingana kimaongezi. na matumizi ya lugha
Sura ya utafiti wetu. tatu, ya nne, na tano ndizo kiini cha
Tunaanza kwa kutoa ya ho j'a za kijumla kutokana
na utafiti wetu. Kisha tunaiainisha data yetu na
kuichanganua katika viwango vya matamshi, sarufi, na
msamiati na maana. Katika kila kiwango na kwa kila kosa
(ukiushi) tunatoa maelezo yanayotokana na utafiti wetu
kuhusu kile kinachosababisha mzungumzaji kulifanya kosa
hilo. Sura ya sita ni hitimisho la kazi hii, ambapo tunatoa
maelezo ya kijumla kuhusu utafiti wetu na matokeo yake.
Pia tumetoa mapendekezo ya utafiti zaidi unaoweza kufanywa
katika uwanja huu wa uchunguzi wa matumizi ya lugha ya
kimaongezi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [625]
The following license files are associated with this item: