Show simple item record

dc.contributor.authorShake, Rose M
dc.date.accessioned2021-09-08T05:22:30Z
dc.date.available2021-09-08T05:22:30Z
dc.date.issued1991
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155442
dc.description.abstractUtafiti huu umetokana na imani ~wa~ba ukiushi katika lugha ya kireaongezi ni tukio halisi na dhahiri katika matumizi ya lugha yo yote ile. (Taz. Max Black, 1968). Kuifahamu lugha na kuielewa kikamilifu kunahusu pia ufahamu wa hali ya ukiushi na sababu za ukiushi huo unaotokea. Tasnifu hii imechunguza na kuonyesha baadhi ya makosa (ukiushi) yanayotokea katika hali halisi ya maongezi ya wahusika kutoka katika mtaa wa Kariobangi South, wjini Nairobi. Kazi hii imegawanywa katika sura sita. Kila sura inajadili kipengee maalum kinachohusu matumizi ya lugha. Kila sura ina utangulizi, na panapo hitajika, kiishio kinachotoa muhtasari na uamuzi wa jumla kulingana na matokeo ya utafiti. Sura ya kwanza ni sura hii unatoa utangulizi wa utafiti. Utangulizi wa maelezo machache kuhusu mtaa wa Kariobangi South (tulikofanyia utafiti) na wakazi ~Jake. Katika sura hii pia tumejadili somo letu la utafiti, madhumuni yetu ya kuufanya utafiti huu na upeo wa tasnifu. Zaidi ya hayo pia tumeelezea kuhusu nadharia tunayoitumia kama kigezo cha kupimia matumizi ya lugha. Katika sehemu ya 'Yaliyofanywa kuhusu somo', tunajadili baadhi ya kazi zingine zilizofanywa na kuandikwa na ~mbazo, kwa namna fulani, zinahusiana na utafiti wetu. Tunatoa sababu zetu za kulichagua so~o katika sura hiyo ya kwanza. Fauka ya hayo, tunatoa maelezo kuhusu haipothesia zinazopimwa katika utafiti huu na njia tulizozitumia katika kuufanya utafiti wetu. Sura ya pili inayashughulikia masiala muhimu kuhusu lugha ya Kiswahili na matumizi yake kwa jumla. Tunaziangalia hoja za usanifishaji wa lugha na dhana ya ukiushi katika matumizi ya lugha; na kuelezea jinsi ambavyo ukiushi unadhihirika kulingana kimaongezi. na matumizi ya lugha Sura ya utafiti wetu. tatu, ya nne, na tano ndizo kiini cha Tunaanza kwa kutoa ya ho j'a za kijumla kutokana na utafiti wetu. Kisha tunaiainisha data yetu na kuichanganua katika viwango vya matamshi, sarufi, na msamiati na maana. Katika kila kiwango na kwa kila kosa (ukiushi) tunatoa maelezo yanayotokana na utafiti wetu kuhusu kile kinachosababisha mzungumzaji kulifanya kosa hilo. Sura ya sita ni hitimisho la kazi hii, ambapo tunatoa maelezo ya kijumla kuhusu utafiti wetu na matokeo yake. Pia tumetoa mapendekezo ya utafiti zaidi unaoweza kufanywa katika uwanja huu wa uchunguzi wa matumizi ya lugha ya kimaongezi.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUkiushi Katika Lugha Ya Kimaongezi Dhidi Yakanuni Za Kiswahili Sanifuen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States