Nafasi Ya Wanawai Katika Uhifadhi Wa Mazinglra Katika Riwaya Ya Nakuruto- Mtazamo Wa Fasihi Ya Ufeministi Wa Kiekolojia
View/ Open
Date
2014Author
Sabula, Millicent A
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Fasihi ya kiekolojia ru uwanja uliochipuka miaka ya 1970 na kuendelea rniaka ya 1990
kuchanganua, kuchambua na kuhakiki kazi za kifasihi. Uwanja huu unalenga kuangazia fani na
maudhui katika matawi ya fasihi kiekolojia kama vile ya Kiafrika, Kimarekani na Kiferninisti.
Utafiti huu unahusu nafasi ya wanawake katika uhifadhi wa mazingira kwa mtazamo wa fasihi
ya ufeministi wa kiekolojia. Lengo kuu la utafiti huu ni kupambanua mchango wa ufeministi wa
kiekolojia katika fasihi ya Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na madhumuni haya: kubainisha
mchango wa ufeministi wa kiekolojia katika uhifadhi wa mazingira katika riwaya ya Nakuruto;
kupambanua mhusika Nakuruto na mchango anaoutoa katika kukabiliana na uharibifu wa
mazingira; kujadili kwa kina changamoto anazopitia mwanawake katika kuhifadhi mazingira;
kujadili athari za masuala ya kirnazingira na jinsi zinavyojitokeza katika riwaya. adharia
iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Ufeministi wa kiekolojia iliyoasisiwa na mfaransa
Francoise d'Eaubonne mwaka wa 1974. Nadharia hii ilibuniwa kwa ajili ya kuleta mapinduzi ya
kiekolojia hasa kwa kumzingatia mwanarnke. Utafiti huu ulifuata muundo wa uchanganuzi wa
makala ambapo maelezo yetu yaliangazia masuala tata yaliyoko kwenye matini tuele. Maka1a ya
kimsingi ya utafiti yalikuwa ni riwaya ya Nakuruto ilhali rnakala ya sekondari yalitokana na
usomaji wa vitabu na makala yaliyohusu mada. Utafiti huu ulibainisha kwamba uferninisti wa
kiekolojia una nafasi ya kuwazindua wanawake ili kuleta ukornbozi wa kimazingira. Aidha,
utafiti ulitambua kuwa mhusika Nakuruto aliwazindua wanajarniikupitia kwa el imu na maarifa
yake ya kimazingira, hivyo kusababisha mapinduzi. Utafiti ulitambua kwamba wanawake
wanasimangwa, kutukanwa, kudharauliwa na kudunishwa wanapojihusisha na harakati za
utunzaji mazingira. Mwisho utafiti ulitarnbua kwarnba umaskini, kukauka kwa chernichemi za
maji, uskwota, magonjwa na vifo ni athari zinazosababishwa na uharibu wa mazingira. Utafiti
huu ulihitimisha kwarnba mwanamke anastahili kupewa nafasi katika uhifadhi wa mazingira na
kwamba, fasihi ya Kiswahili ina uwezo wa kumulika masuala ya kielokojia kama
yanavyojitokeza katikajamii. Kwa kuwa utafiti huu haukuweza kuchunguza vipcngele vyote vya
kifasihi mazingira, mtafiti anapendekeza kwamba utafiti wa baadaye uzingatie mikabala minginc
kama vile fasihi mazingira kieneo, Kiafrika na Kimagharibi, hasa kwa mkondo wa kilinganishi.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [657]
The following license files are associated with this item: