Show simple item record

dc.contributor.authorMungai, Paul K
dc.date.accessioned2021-09-08T08:02:30Z
dc.date.available2021-09-08T08:02:30Z
dc.date.issued2005
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155449
dc.description.abstractTasnifu hii ni juu ya uhakiki-linganishi wa ki-fani wa tenzi za Swifa ya Nguvumali (5 Y N M) na Mikidadi na Mayasa(M N M). Utenzi wa M N M ulitungwa na SaidAbdallah Masudiel Buhry miaka mingi kabla ya Karne ya Ishirini. Utenzi huu umetafsiriwa kwa Kiingerezana J.W. Allen (1971) lakini haujafanyiwa uhakiki wa aina yoyote. Unasimulia juu ya mashujaa wawili wa Kiislamu, Mikidadi na Mayasa na jinsi walivyoshinda pingamizi walizowekewa na baba yake Mayasa ili wasioane. Utenzi wa SY N M ulitungwa na Bwana Hasan bin Ismail (1968). Umehaririwa na kutarjumiwa kwa Kiingereza na Peter Lienhardt (1968). Utenzi huu umefanyiwa utafiti na Prof. M. H. Abdulaziz (1J.6~), allyehaklki matumizi ya lugha. Utafiti huo uliendelezwa na E. Kadenge Kazungu (1982) aliyehakiki ukiushi wa kaida za lugha katika utenzi huu. Katika uchunguzi wake, E. K. Kadenge amekipa kipengele cha tamathali za us~mi nafasi muhimu. Utafiti wetu umeenda mbali kwa kuvihakiki vipengele vyote vya fani kama vile wahusika, mtindo, muundo, ploti, mandhari na kuvilinganisha katika tenzi husika. Kwa.hivyo, tutalinganisha tenzi hizi mbili kifani kwa kuangalia jinsi fani yake inavyolingana au kutofautiana kwa kuzingatia kuwa tenzi hizi zilitungwa kwa nyakati na mazingira mbalimbali. Mwongozowetu katika tasnifu hii ni nadharia ya Urasrntambayo huangalia ~ fasihi kama sanaa ya maneno. Tumelinganisha fani na vipengele vyake katika tenzi hizi mbili kwa kutambulisha kila mojawapo na kuchanganua maana na uamilifu wake katika muktadha wa matumizi. Kazi yetu imegawanywa katika sura nne. Sura ya kwanza ni utangulizi unaoelezasomo la utafiti, madhumuni ya tasnifu, sababu za kuchagua somo hili, madhumuni ya somo, upeo na mipaka, msingi wa nadharia, nadharia tete na njia tulizotumia kufanyia utafiti huu. Katika sura hii pia tumerejelea kazi mbalimbali zilizofanywa kuhusu somo hili. Katika sura ya pili tumejadili dhana ya fani. Tumeshughulikia vipengele vya fani kwa kurejelea wataalamu na wahakiki mbalimbali pamoja na maoni yetu juu ya kunga hizo. Katika sura ya tatu tumelinganisha kila mojawapo ya vipengele vya fani vinavyojitokeza katika tenzi za M N M na S Y N M. Sura ya nne ni hitimisho ambapo tumeelezea pale tulipofikia katika utafiti wetu. Katika sura hii pia tumetathimini haipothesia ya utafiti wetu pamoja na kuonyesha kama tumeweza kuifikia au la. Vilevile tumetoa mapendekezoyetu.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUhakiki Linganishi Wa Kifani Wa Tenzi Za Mikidadi Na Mavasa Na Swifa Va Nguvumalien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States