dc.description.abstract | Tasnifu hii imeshughulikia mtindo katikaArusi ya Buldoza na Hadithi Nyingine. Tasnifu
hii ina sura tano.
Katika sura ya kwanza, tumegusia tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za
kuchagua mada, nadharia tete,upeo na mipaka ya utafiti, yaliyoandikwa kuhusu mada ya
utafiti, msingi wa nadharia ya utafiti na njia tulizotumia katika utafiti huu.
Kuhusu sura ya pili, tumechanganua mtindo wa sintaksia katika Arusi ya Buldoza na
Hadithi Nyingine. Tumejadili ukiushi wa vipashio katika sentensi, urefu na ufupi wa
sentensi na nafasi ya uakifishi katika sintaksia ya diwani yenyewe.
Sura ya tatu imeangazia ukiushi wa kisemantiki katika diwani ya Arusi ya Buldoza na
Hadithi Nyingine. Tumechambua matumizi ya methali, semi, tamathali za usemi na
mbinu nyingine za lugha.
Katika sura ya nne, tumeshughulikia matumizi ya msamiati kwa jumla katika Arusi ya
Buldoza na Hadithi Nyingine. Tumechunguza namna mwandishi alivyoteua msamiati
wake iIi kuwasilisha ujumbe wake.
Sura ya tano ina hitimisho la utafiti. Pia, imegusia umuhimu wa utafiti huu na kutoa
mapendekezo ya utafiti wa baadaye katika diwani ya Arusi ya Buldoza na Hadithi
Nyingine. | en_US |