dc.description.abstract | Lengo kuu la utafiti huu limekuwa ni kubainisha Jll1Sl taswira durnifu za uana
zinavyojitokeza katika fasihi ya Kiswahili ya watoto.
Nadharia tete tatu zilizoongoza utafiti huu ni: Mosi, taswira dumifu za uana zinadhihirika
katika fasihi ya Kiswahili ya watoto. Pili, wahusika katika fasihi ya Kiswahili ya watoto
husawiriwa kwa njia sawa bila kubaguliwa kwa misingi ya jinsia zao. Mwisho, waandishi
wa kazi za fasihi ya Kiswahili ya watoto huwakilisha idadi sawa ya wahusika wa kike na
kiume katika kazi hizo. Kupitia kwa utafiti huu, nadharia tete ya kwanza imethibitishwa
kuwa kweli. Lakini nadharia tete ya pili na ya tatu zimethibitishwa kuwa si kweli.
Mikabala ya uana na ufeministi ambayo imetumika katika utafiti huu ilitoa msingi
madhubuti katika utafiti huu ila tulilazimika kuitumia kwa tahadhari kwa sababu inaakisi
rnno tamaduni za Kimagharibi. Kuna juhudi zinazofanywa za kutafuta mkabala wa
ufeministi unaoafiki zaidi uhakiki wa fasihi ya Kiafrika.
Tasnifu hii ina sura tano zinazoshughulikia kipengele cha taswira dumifu za uana katika
fasihi ya Kiswahili ya watoto ifuatavyo:
Sura ya kwanza inatoa kwa ujumla mwelekeo wa kuchunguza jinsi taswira dumifu za
uana zinavyoweza kudhihirishwa katika fasihi ya Kiswahili ya watoto. Inahusisha
sehemu kuhusu somo la utafiti, malengo, nadharia tete, sababu za kuchagua somo hili,
yaliyoandikwa kuhusu somo hili, msingi wa kinadharia, upeo na mipaka na njia za utafiti.
Sura ya pili irnejadili kwa ujumla kuhusu Iasihi ya watoto, sifa na majukumu yake.
tofauti kati ya dhana 'uana' najinsia. Aidha sura hii irnezungumzia taswira dumifu.
Katika sura za tatu na nne, tumechunguza matini za tungo za fasihi ya Kiswahili ya
watoto za waandishi wa kiume (androtexts) na kike (gynotexts) mtawalia ili kubainisha
jinsi taswira dumifu za uana zinavyojitokeza. Kadhalika katika sura hizi, tumechunguza
iwapo wahusika wa kike na kiume wamewakilishwa kwa idadi sawa kwenye matini hizo.
Sura ya tano ni hitimisho. Ina sehemu za muhtasari wa matokeo ya utafiti huu kwa
misingi ya nadharia tete zilizoongoza uchunguzi huu, matatizo tuliyokumbana nayo
katika utafiti huu na mapendekezo kuhusu utafiti zaidi. | en_US |