Show simple item record

dc.contributor.authorNgunjiri, Dadson M
dc.date.accessioned2021-09-09T05:42:04Z
dc.date.available2021-09-09T05:42:04Z
dc.date.issued2012
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155455
dc.description.abstractSomo letu la utafiti linashughulikia matumizi ya taswira kama kigezo cha kufanikisha maudhui katika Utendi wa Siiraji. Utafiti wetu unanuia kuchunguza kigezo cha taswira na umuhimu wake katika kufanya maudhui ya mtunzi yawe ya kutambuliwa na kuthaminika na msomi . Kwenye sura ya kwanza tumechunguza masuala; Mwanzo tumetanguliza kuhusu mada tunayoshughulikia, tatizo la utafiti, nadharia tete, umuhimu wa kushughulikia mada, upeo na mipaka, yaliondikwa kuhusu Utendi wa Siiraji, msingi wa nadharia na njia ya utafiti. Taswira tunayoishughulikia ni taswira chanya inayofungamanishwa na maudhui ya utendi tunaouhakiki. Sura ya pili inahusu historia ya mwandishi. Sura hii inatoa maisha ya mtunzi, Muhammadi Kijumwa kwenye daraja zifuatazo; asili yake, elimu, ndoa yake, ndoa ya Kiislamu, Ndoa ya Kikristo, asasi halisi ya mtunzi, mchango wake kwenye uwanja wa fasihi, kazi alizozitunga, kazi alizozinakili, kazi alizotafsiri, nyimbo alizotunga, tutumbi na barua alizoandika, uhusiano wake na wageni na pia wenyeji, dini na imani ya mtunzi. Sura ya tatu imeshughulikia dhana ya talaka kwa mjibu wa dini ya Kikristo, Kiislamu, dhana ya maadili kwenye tungo za kishairi, na dhana ya taswira. Sura ya nne ndiyo upeo wa utafiti wetu kwani inashughulikia asili ya Utendi wa Siiraji, dhana ya maudhui kwenye utendi na jinsi kigezo cha taswira kimeunganishwa na maudhui. Maudhui makuu yanayojitokeza kwenye utendi kama vile; ushirikiano, ukarimu, tabia njema, usiri, suluhisho na mapatano, asasi ya ndoa, bidii, wema na utu, Mwisho ni sura ya tano, ambayo inasheheni hitimisho la kazi nzima na mapendekezo kuhusu uhakiki uliyo shughulikiwa. Ni sura hii ambayo imependekeza kazi kadhaa ya utafiti wa ziada.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleMatumizi Ya Taswira Kama Klgezo Cha Kufanikisha Maudhui Katlka Utendi Wa Siiraji Uliyotungwa Na Muhammad I Kijumwaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States