Show simple item record

dc.contributor.authorMiricho, Erastus M
dc.date.accessioned2021-09-13T05:43:49Z
dc.date.available2021-09-13T05:43:49Z
dc.date.issued2015
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155462
dc.description.abstractMada ya utafiti huu ilikuwa kuchunguza usawiri wa watoto katika hadithi za Mwepesi vva Kusahau na Likizo ya Mkosi. Hadithi hizi za watoto zimejikita katika fasihi ya watoto. Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kubainisha taswira za mtoto wa kike na zile za mtoto wa kiume, kulinganisha sifa za watoto wa kike na wenzao wa kiume na kuchunguza mitazamo ya watoto wa kike kuhusu wenzao wa kiume katika Mwepesi lin Kusahau na Likizo ya Mkosi. Nadhariatete mbili zilizoongoza utafiti huu ni kwamba katika hadithi za watoto msichana huchorwa akiwa mwema kuliko mvulana na pili ni kuwa wasichana na wavulana katika jamii ya sasa wanajiona kuwa sawa. Nadharia ya sosholojia ya fasihi iliyotumiwa katika utafiti huu ilitoa msingi madhubuti wa kutathiminia usawiri wa watoto wa kike na wale wa kiume kwa vile imethibitika kuwa usawiri unaobainika unafungamana na hali ilivyo katika maisha ya jamii ya kame hii ya ishirini na moja ambapo inadaiwa wasichana wanaendelea kuwapiku wavulana katika nyanja mbalimbali za kijamii zikiwemo elimu na maadili. Matokeo ya utafiti huu yamethibitisha kuwa katika jamii ya mwandishi mtoto wa kike anasawiriwa kwa njia chanya zaidi kuliko mtoto wa kiume. Rata hivyo, imedhihirika kuwa watoto wenyewe hawachukiani baina ya wale wa kike na wale wa kiume. Kupitia kwa utafiti huu nadhariatete zote mbili zilithibitishwa kuwa kweli. Msichana amechorwa kama aliye mwema kuliko mvulana. Imethibitishwa pia kuwa katika kame ya ishirini na moja hakuna majukumu wanayotengewa wasichana ama wavulana pekee bali wavulana na wasichana wanashirikiana kufanya kazi zozote. Mapendekezo yametolewa kuwa kuna haja ya kuchukua hatua za dharma kushughulikia maslahi ya mtoto wa kiume katika jamii. Jambo hili litamwokoa kutokana na hatari ya kubaki nyuma ya mtoto wa kike katika elimu na shughuli nyingine za kijamii. Mwishowe, tumetoa mapendekezo ya utafiti zaidi.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleUsawiri Wa Watoto Katlka Hadithi Za Mwepesi Wa Kusaha Unalikizo Ya Mkosien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States