dc.contributor.author | Ndung'u, Mary N | |
dc.date.accessioned | 2021-09-13T09:26:42Z | |
dc.date.available | 2021-09-13T09:26:42Z | |
dc.date.issued | 2009 | |
dc.identifier.uri | http://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/155466 | |
dc.description.abstract | Utafiti huu umeshughulikia mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu. Tumechunguza na
kuchanganua tungo ambazo hutambulisha mada na fokasi huku tukitolea maelezo na
ufafanuzi wa kina, Malengo ya utafiti huu ni kuchunguza ikiwa kuna uhusiano kati ya
mada na fokasi. Pia tumechunguza utambulishaji wa mada na fokasi huku tukitathmini
ikiwa mada na fokasi huweza kutambulishwa kwenye kirai. kishazi au kileksika. Mwisho
tumetathmini kufanikiwa kwa Mtazamo wa Muundo wa Taarifa katika utarnbulishaj i wa
mada na Iokasi katika Kiswahili Sanilu.
Nadharia ambayo imetuongoza katika utafiti huu ni Mtazamo wa Muundo wa Taarifa
iliyoasisiwa na Wanaisimu wa Shule ya Prague, ikaendelezwa na Halliday (1967) na
baadaye kukuzwa zaidi na Lambrecht (1994), Muundo wa taarifa husimbwa katika
sentensi katika utambulishaji wa mada na fokasi ili kubainisha ni sehernu gani ya seniensi
inayobeba taarifa mpya na ni sehemu gani inayobeba taarila inayojulikana.
Katika uchanganuzi wa data. tumeteua data kutoka riwaya ya f\1I1i ya Adam Shafi (1979)
ambayo tumetumia kama data ya kimsingi. Aidha tumepata data zaidi kutoka makala
mbalimbali zilizochapishwa. Zaidi ya hayo tumezalisha data ili kukidhi mahitaji yetu
katika uchanganuzi wa tungo ambazo hutarnbulisha mada na fokasi katika Kiswahili
Sanifu.
Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti huu. lmejumlisha utangulizi. mada ya utafiti.
madhumuni ya utafiti. nadharia tete. sababu za kuchagua mada hii. upeo na mipaka.
uhalalishaji. msingi wa kinadharia. yaliyoandikwa kuhusu mada ya utafiti na mbinu za
utafiti.
Sura ya pili imeshughulikia maswala ya kimsingi yanayohusiana na mada, fokasi na
msingi wa kinadharia wa Muundo wa Taarifa. Katika sura ya tatu. tumeshughulikia na
kuchanganua tungo ambazo hutambulisha mada. Tumepata kuwa mada katika sentensi
huhitaji kuakisiwa kama vile katika kuitanguliza katika sentensi. kuihamislia kushoto
. . . . . .
rruongoru mwa njia zingme.
Sura ya nne imejikita katika uchanganuzi wa clata katika tungo ambazo hutambulisha
fokasi katika Kiswahili Sanifu. Tumechunguza aina za Iokasi kama vile fokasi kwenye
kiarifu, Iokasi kwenye KN na fokasi katika senteusi miongoni mwa aina zingine za
Iokasi.
Katika sura ya tano. tumeangalia jinsi mada na fokasi huhusiana katika muktadha wa
utambuzi. uchochezi. na ulinganuzi. Tumepata kuwa mpangilio wa rnaneno katika
sentensi huwa na mchango mkubwa katika utambulishaji wa mada na fokasi katika
Kiswahili Sanifu arnbao huwa huru kwa kiasi.
Sura ya sita inabeba hitimisho na mapendekezo ya utafiti huu. Katika hitimisho tumetoa
matokeo ya utafiti yanayohusiana na utambulishaji wa mada na Iokasi katika Kiswahili
Sanifu. Mapendekezo ambayo tumetoa yatachochea tafiti zaidi katika uwanja huu.
Tumependekeza kuwa tafiti zaidi zifanywe katika uchanganuzi wa data \\\:1
kimofosintaksia katika utambulishaji wa mada na fokasi katika Kiswahili Sanifu. Pia
tafiti zaidi ambazo zitaongozwa na nadharia tofauti au utafiti katika usimbaji wa rnuundo
wa taarifa kwenye tungo changamani za kimofosintaksia au za kiarudhi | en_US |
dc.language.iso | other | en_US |
dc.publisher | University of Nairobi | en_US |
dc.rights | Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States | * |
dc.rights.uri | http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/ | * |
dc.title | Mada Na Fokasi Katika Kiswahili Sanifu: Mtazamo Wa Muundo Wa Taarifa. | en_US |
dc.type | Thesis | en_US |