Ukuaji Wa Muundo Na Mawazo Katlka Tamthilia Za Timothy Arege Mtazamo Wa Umuundo
View/ Open
Date
2013Author
Ndege, Charles M
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu umechunguza ukuaji wa muundo na mawazo katika tamthilia za Timothy
Arege. Tamthilia zilizoteuliwa kuhakikiwa ni tatu. Nazo ni: Chamchela (2007), Kijiba
cha Moyo(2009) na Mstahiki Meya (201 1)
Sura ya kwanza ni utangulizi, tatizo la utafiti, madhumni ya utafiti, nadharia tete, upeo na
mipaka na msingl wa nadharia. Pia, tumejumuhisha yaliyoandikwa kuhusu mada, na
mbinu za utafiti zizotumika katika kazi hii.
Sura ya pili imeshughulikia msuko kama mojawapo wa vipengele vya muundo na
mchango wake katika tamthilia za Arege. Tumetanguliza kwa kuangazia dhana ya
msuko, kanuni za ploti pamoja na mchango wao katika kuendeleza ukuaji wa muundo na
mawazo katika tamthilia za Arege.
Sura ya tatu imeangazia mchango wa wahusika katika kuendeleza dhamira na maudhui.
Tumeshughulikia majukumu yao na mchango wao katika kuibua maudhui na dhamira.
Sura ya nne nayo imeshughulikia mchango wa matumiii ya lugha katika kudhihirisha
ukuaji wa muundo na mawazo katika tamthilia za Arege. Tumeshughulikia tamathali za
lugha kama vile tashihisi, balagha, uzungumzinafsia, kuchanganya ndimi, tashbihi,
dhihaka, methali, mdokezo, sitiari na kinaya.
Sura ya tano inatoa muhtasari wa matokeo ya utafiti na mapendekezo ya tafiti za
baadaye.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [646]
The following license files are associated with this item: