Uhalisiajabu unavyojitokeza katlka ukawafi wa Miiraji na utenzi wa Fumo Liyongo
View/ Open
Date
2016Author
Onchwati, Jared, S
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu ulikusudia kuonyesha sifa za kiuhalisiajabu kama zinavyojitokeza katika
Ukawafi wa Miiraji na Utenzi wa Fumo Liyongo. Tulifanyanya hivyo kwa
kuwarejelea baadhi ya wahusika na mandhari kama yalivyosawiriwa katika tcnzi
zenyewe. Madhumuni yetu katika utafiti huu yalikuwa kudhihirisha uhalisiajabu
ulivyosawiriwa katika tenzi. Aidha tulibaini kuwa sifa za kiuhalisiajabu zilikuwa
nguzo muhimu kwa watunzi wa tenzi hizi katika kufikia malengo yao mbali na wao
kutengana kiwakati na kiumri.
Tuliufikia uchanganuzi huu baada ya kutambua kuwa, uhalisiajabu katika tenzi
haujatafitiwa sana ilihali ni mojawapo ya fasihi kongwe zaidi kuliko riwaya na
tamthilia. Tumeangalia sifa za takribani wahusika wote katika tenzi hizi, mazingira
walimolelewa pamoja na jamii zilizowazaa na kuwalea. Vile vile tumeangalia
umuhimu wao katika jamii zao. Data ilikusanywa maktabani, mtandaoni na
kuchanganuliwa kwa misingi ya nadharia ya uhalisiajabu iliyoasisiwa na Franz Roh
( 1925).
Matokeo ya utafiti wetu yalilingana na nadharia tete zilizoongoza mchakato mzima
wa utafiti wetu. Kupitia kwa sifa za wahusika na za mandhari tuligundua kuwa tenzi
zimesheheni uhalisiajabu sawia na vipera vingine vya fasihi. Mbali na tenzi zote mbili
kudhihirisha sifa za kiuhalisiajabu, ilidhihirika kuwa dhamira za watunzi wa tenzi hizi
zimetofautiana mno. Tuligundua kuwa uhalisiajabuhusawiriwa vyema katika
mandhari, wahusika wenye sifa za kibinadamu na wale wasiokuwa na sifa za
kibinadamu. Aidha tulibaini kuwa wahusika wa aina hizi zote, ni sehemu muhimu
katika kujenga historia yajamii zao na dunia yote kwa ujumla.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
The following license files are associated with this item: