Show simple item record

dc.contributor.authorMbae, Patrick N
dc.date.accessioned2022-05-10T10:01:52Z
dc.date.available2022-05-10T10:01:52Z
dc.date.issued2021
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/160478
dc.description.abstractUpole na utoupole ni dhana za kimsingi sana katika mchakato mzima wa mawasiliano. Kufaulishwa na kudumishwa kwa mawasiliano hutegemea jinsi dhana hizi zinavyoshirikishwa katika mazungumzo. Wanapragmatiki wametambua kuwa watumizi lugha hutumia dhana hizi kimakusudi kutekeleza azma mahususi za kimawasiliano. Tabia za upole hutumiwa pale ambapo mzungumzaji analenga kuhifadhi nyuso za wasikilizaji huku tabia za utoupole zikitumiwa pale ambapo vitendo vya kimazungumzo vinaelekezwa katika kudhuru nyuso za wasikilizaji. Tasnifu hii inadhamiria kuonyesha nafasi ya utoupole katika kuleta mabadiliko ya kijamii kama inavyobainika katika riwaya ya Mtoto wa Mama ya Adam Shafi. Matokeo ya utafiti huu yataonyesha iwapo uamuzi wa wahusika kutumia lugha ya utoupole unachochewa na masiala yoyote ya kijamii pamoja na kuonyesha mabadiliko ya kijamii ambayo yanatokana na maamuzi hayo ya kutoa kauli au vitendo vya utoupole. Utafiti huu utatumia nadharia ya utoupole ya Culpeper (1996) ili kutambua ni kauli zipi na za wahusika wepi ambazo zinadhihirisha utoupole. Matokeo ya utafiti huu yatakuwa mwongozo mzuri kwa watafiti wa baadaye ambao wangependelea kuchunguza utoupole katika tanzu nyinginezo za fasihi andishi kama vile ushairi, hadithi fupi na tamthilia.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.titleNafasi Ya Utoupole Katika Kusababisha Mabadiliko Ya Kijamii: Uchanganuzi Wa Riwaya Ya Mtoto Wa Mama Ya Adam Shafien_US
dc.typeOtheren_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States