Show simple item record

dc.contributor.authorKamwara, Kawira
dc.date.accessioned2023-07-14T06:17:12Z
dc.date.available2023-07-14T06:17:12Z
dc.date.issued2022
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke/handle/11295/163721
dc.description.abstractJamii nyingi za Kiafrika ni za kuumeni na humweka mwanamke katika ngazi za chini akilinganishwa na mwanamume. Utafiti huu ulishughulikia mchango wa waandishi katika kuangazia jitihada za mwanamke katika kujijengea ujitambuzinafsia wake katika jamii. Hili limewezekana kupitia mada ”Ujenzi wa Ujitambuzinafsia wa Jinsia na Upembezwaji wa Mwanamke katika Bunilizi teule za Clara Momanyi na Omar Babu”. Bunilizi za Clara Momanyi ni; ‘Ngome ya Nafsi’ (2004), Tumaini (2006) na Nakuruto (2009) nazo za Babu ni Kala Tufaha (2007), Heri Subira (2010) na ‘Ndoa ya Samani’ (2011). Umuhimu wa utafiti huu umekuwa kuonyesha jinsi mwanamke anavyopembezwa katika jamii kisanii hasa kutokana na mitazamo ya kiitikadi ya watunzi hawa wawili katika bunilizi zao. Licha ya hayo, tunatazamia kuwafaidi watetezi wa haki za binadamu katika harakati zao za kuihamasisha jamii kuhusu upembezwaji wa mwanamke katika jamii. Mbali na hayo, tumekusudia utafiti huu uweze kuwapa mshawasha wahakiki na wasomi kuzitafiti kazi nyingine za kifasihi ili kutoa picha ya mwanamke anayepembezwa kisanii katika jamii. Isitoshe, utafiti wetu utatumika kama hazina muhimu ya marejeleo kwa watafiti wa masuala ya kijinsia wa siku zijazo katika kuendeleza tafiti zao. Nadharia tuliyotumia ni ya Ubaada wa Ufeministi wa Kiafrika. Mwasisi mkuu wa nadharia hii ni Steady (1981) aliyesema kuwa Ubaada wa Ufeministi wa Kiafrika huweka pamoja masuala ya kijinsia, ubaguzi, mielekeo ya kiutamaduni na kitabaka ili kumwangalia mwanamke kama kiumbe mtagemewa bali sio mtegemezi. Mbinu ya sampuli ya kimaksudi ilitumika kusampuli bunilizi hizi ili kukusanya data maktabani na kisha kuichanganua na kuiwasilisha kimaelezo. Uchanganuzi huu ulifanyika ili kufanikisha madhumuni ya utafiti huu ambayo ni; kuchanganua kwa kina jinsi ujenzi wa ujitambuzinafsia wa jinsia na upembezwaji wa mwanamke unavyojitokeza kisanii katika tungo za watunzi hawa wawili, kuchunguza athari za mazingira katika ujenzi wa ujitambuzinafsia wa jinsia na upembezwaji wa mwanamke, kutathmini udhihirikaji wa mitazamo ya watunzi hawa wawili kuhusu ujitambuzinafsia wa jinsia na upembezwaji wa mwanamke na kubainisha athari za mitazamo ya watunzi hawa katika usawiri na ujenzi wa ujitambuzinafsia wa jinsia na upembezwaji wa mwanamke katika bunilizi zao. Tasnifu hii imegawanywa katika sura sita. Sura ya kwanza ni utangulizi wa utafiti ambapo mada ya utafiti, madhumuni ya utafiti, sababu za kuchagua mada, upeo na mipaka, yaliyoandikwa kuhusu mada, misingi ya kinadharia, njia za utafiti, uteuzi wa sampuli pamoja na ukusanyaji wa data. Sura ya pili ni ujenzi wa ujitambizinafsi kama unavyojitokeza katika bunilizi za Momanyi na Babu. Katika sura ya tatu tumejikita katika utamaduni na ubabedume kama mihimili ya ujitambuzinafsia. Sura ya nne ni utetezi wa haki za mwanamke na ujitambuzinnafsi wa jinsia. Katika sura ya tano, tumeangazia ulinganishi na ulinganuzi wa maudhui ya ujenzi wa ujitambuzinafsia wa jinsia katika bunilizi teule za Clara Momanyi na Omar Babu. Hatimaye, sura ya sita ni muhtasari, mahitimisho na mapendekezo ya utafiti huu.en_US
dc.language.isoothersen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.rightsAttribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States*
dc.rights.urihttp://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/*
dc.subjectUpembezwaji Wa Mwanamke Katika Bunilizi Teule Za Clara Momanyi Na Omar Babuen_US
dc.titleUjenzi Wa Ujitambuzinafsia Wa Jinsia Na Upembezwaji Wa Mwanamke Katika Bunilizi Teule Za Clara Momanyi Na Omar Babuen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail
Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States
Except where otherwise noted, this item's license is described as Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United States