Kuathirika Kwa Kiswahili Kutokana Na Ubadilishaji Msimbo Katika Mawasiliano Ya Biashara: Kifani Cha Diskosi Ya Jua Kali, Soko La Daraja Mbili, Kisii
View/ Open
Date
2023Author
Orucho, Seraphine K
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Utafiti huu ulikusudia kuchanganua na kujadili kuathirika kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili kutokana na ubadilishaji msimbo katika mazungumzo kati ya wauzaji na wanunuzi katika soko la wazi la Daraja Mbili, mjini Kisii.
Soko la Daraja Mbili lilitumika kama kifani cha uhalisia wa ubadilishaji msimbo unaoathiri matumizi ya lugha ya Kiswahili katika masoko ya wazi nchini Kenya, yanayowakutanisha watu kutoka jamii-tumizi lugha mbalimbali.
Hata kama soko la Daraja Mbili linaweza kuangaliwa kama soko la kieneo, uchakataji wa data kuhusiana na ubadilishaji msimbo katika soko hili unaakisi ukweli wa ubadilshaji msimbo katika masoko yote ya nchi ya Kenya.
Zaidi ya hayo uchakataji wa data ulituwezesha kuafikia malengo ya utafiti huu ya kuchanganua visababishi na vichochezi vya ubadilishaji msimbo, aina za ubadilishaji msimbo na hatimaye athari hasi na chanya za ubadilishaji msimbo katika soko la Daraja Mbili mjini Kisii.
Publisher
University of Nairobi
Rights
Attribution-NonCommercial-NoDerivs 3.0 United StatesUsage Rights
http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/Collections
- Faculty of Arts [770]
The following license files are associated with this item: