Show simple item record

dc.contributor.authorGichamba, Julius M
dc.date.accessioned2013-05-02T11:57:35Z
dc.date.available2013-05-02T11:57:35Z
dc.date.issued2005
dc.identifier.citationIdara Ya Isimu Na Lugha Chuo Kikuu Cha Nairobien
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18381
dc.description.abstractTasnifu hii inajumlisha matokeo ya utafiti wetu uliolenga kuzipambanua sifa za kishujaa za Furno Liyongo na Shaka Zulu pamoja na kuelezea umuhimu wa mashujaa hawa kwa jamii zao. Tumeibawibu tasnifu hii katika faslu tano kila mojawapo ikishughulikia kipengele fulani maalum. Hata hivyo, vipengele vyote vilivyomo vinaingiliana na kukami lishana. Faslu ya kwanza ni usuli wa tasnifu. Katika faslu hii, tumeelezea masuala muhimu na ya kijumla kuhusiana na mchakato mzima wa utafiti. Tumetanguliza kwa kuifasili dhana ya shujaa na kutoa mifano ya baadhi ya mashujaa duniani miongoni mwa masuala mengine ya kijumla kuwahusu majagina. Pia, tumelifafanua somo la utafiti na kisha tukaelezea madhumuni na nadharia tete za utafiti wetu. Ni katika faslu hii ambapo tumezielezea sababu za kulichagua somo pamoja na kufafanua nadharia ambazo zimetuongoza katika mchakato mzima wa utafiti wetu. Hatimaye, tumezielezea njia za utafiti ambazo tulizitumia kupata data ili kutekeleza madhumuni ya utafiti wetu. Faslu ya pili inalenga katika kufafanua salua ya Furno Liyongo na Shaka Zulu kwa kuifungamanisha na salua ya jamii zao; yaani, ile ya Waswahili na ya Wazulu. Katika kuelezea salua ya jamii hizi, tumelenga katika kuyafafanua mazingira ya kitamaduni (ya kijamii, kisiasa na kiuchumi). Majagina huwa hawazuki katika ombwe tupu na kwa hiyo lengo hasa la faslu hii ni kutoa taswira ya mazing ira, hali za kijamii na kipindi ambacho Shaka Zulu na Furno Liyongo walizuka pamoja na kuelezea masuala muhimu katika maisha yao. Faslu ya tatu inatalii kiulinganishi sifa za kishujaa za F4mO Liyongo na Shaka Zulu. Tumezifafanua kwa undani sifa zao za kishujaa huku tukionyesha kiwango cha kushabihiana na kutofautiana kwa sifa hizi. Faslu ya nne inafafanua umuhimu wa Furno Liyongo na Shaka Zulu kwa jamii zao. Tumeitazama 'taasisi ya shujaa' kama taasisi nyingine yoyote katika jamii ambayo huzuka iii kutekeleza mahitaji fulani katika jamii. Ni kutokana na kuyatimiza mahitaji haya ndiposa umuhimu wao umedhihirika. Faslu ya tano inajumlisha hitimisho ya tasnifu na mapendekezo kuhusu utafiti wa ziada. Tumetalii kwa kifupi masuala ya kijumla na hususa yanayohusu matokeo ya utafiti wetu na kisha tukapendekeza baadhi ya masuala ambayo watafiti wa halafu wanaweza wakatalii.en
dc.language.isoenen
dc.titleSifa za mashujaa na umuhimu wao kwa jamii zao: ulinganisgi wa fumo Liyongo na Shaka Zuluen
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment of Kiswahilien


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record