Kiswahili katika shule za upili chini ya mfumo wa 8-4-4:- utafiti katika jiji la Nairobi
Abstract
Tasnifu hii ni utafiti juu ya Kiswahili katika shule za upili
chini ya mfumo wa 8-4-4 uliofanyiwa katika jiji la Nairobi.
Madhumuni yake ni kuangalia masiala yanayohusu, Kiswahili katika
shule za upili chini ya mfumo wa 8-4-4.
Imegawanyika katika sura nne. Katika sura ya kwanza kuna mada
ya tasnifu, madhumuni ya tasnifu, sababu za kuchagua somo,
upeo wa kazi hii, msingi wa kinadharia, ya1iyoandikwa kuhusu
swa1a hili, njia za utafiti, matatizo ya utafiti, njia za
kuchagua sampuli na mwisho haipothesia.
Sura ya pili ni maelezo juu ya sera za lugha ya elimu nchini
Kenya kabla na baada ya uhuru, Kiswahili Katika mfumo wa 8-4-4
na vile vile mambo yapaswayo kuzingatiwa katika utekelezaji wa
mradi mpya. Katika kazi hii tutatilia maanani somo la
Kiswahili.
Sura ya tatu ni matokeo ya utafiti kwa jumla. Ina matokeo ya
hojaji na uchanganuzi wa data. Pamoja na rnatatizo na
yanayokikabili Kiswahili na matatuzi yake •
Sura ya nne, ni hitimisho ambayo zaidi ni rnaoni na mapendekezo
ya mtafiti juu ya maswali mbali mbali yanayotokana na data
Lli.yokusanywa katika utafiti.
Marejeo yametolewa baada ya sura ya nne na rnwi.shokabisa ni
nakala ya hoj aj iliyotumiwa kama kiongezo.
Publisher
Department of Linguistics and African Languages, University of Nairobi
Description
'Master of Arts'