dc.description.abstract | Tasnifu hii imechunguza athari za udhanaishi katika riwaya mbili ambazo ni Kichwamaji na
Nguvu ya Sala. Kazi yenyewe imegawika katika sura nne.
Katika sura ya kwanza tumetanguliza kwa ufupi dhana ya udhanaishi. Vilevile, tumebainisha
tatizolinalotafitiwa, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, sababu za kuchagua mada, pamoja na
njiaza utafiti. Aidha tumeangazia udurusu wa kazi mbalimbali pamoja na msingi wa kinadharia.
Tumetumianadharia ya kisosholojia inayosisitiza umuhimu wa mazingira yaliyoibusha kazi ya
msann.
Katika sura ya pili, tumeonyesha athari za udhanaishi zinazobainika katika riwaya ya
Kichwamaji. Vilevile mazingira mbalimbali ambayo yamemwathiri Kezilahabi na kumfanya
achukuemtazamo wa kidhanaishi yamejadiliwa.
Suraya tatu imeangazia udhanaishi katika Nguvu ya Sala. Tumebainisha athari za udhanaishi
kupitia maudhui mbalimbali. Aidha tumeonyesha vile ambavyo mwandishi ameathiriwa na
mazingiraalimoandikia.
Sura ya nne ni hitimisho. Tumehitimisha kwa kutoa maom kuhusiana na kazi hii kwa
ujumla.Vilevile, tumetoa mapendekezo ya utafiti zaidi. | en |