dc.description.abstract | Katika tasnifu hii tumeshughulikia riwaya zaLa peste (1947) ya Albert Camus na
Kichwamaji ya Euphrase Kezilahabi. Tumeangaziajinsi waandishi hao wameshughulikia
maswala ya udhanaishi na fumbo la Mungu kwa jumla.
Uhakiki wetu umegawanywa katika sura tano. Katika sura ya kwanza, tumeelezea tatizo
la utafiti, sababu za kuichagua mada hii, mipaka na upeo na yaliyoandikwa kuhusu
maswala ya udhanaishi na fumbo la Mungu. Kadhalika tumeelezea msingi wa nadharia
iliyotumika katika utafiti huu. Vile vile tumeelezea njia tulizozitumia katika utafiti wetu.
Katika sura ya pili, tumeangalia mukhtasari wa riwaya yaKichwamaji, mikinzano
iliyomo ya kimitazamo pamoja na dhana ya Mungu. Tumeonyesha jinsi mwandishi wa
riwaya hii alivyosawiri swala la udhanaishi na dhana ya Mungu hususan kwa kuzingatia
tofauti za kielimu na vizazi.
Katika sura ya tatu, tumeshughulikia mukhtasari wa riwaya yaLa peste, mikinzano
iliyomo na dhana ya Mungu. Tumeonyeshajinsi mwandishi wa riwaya hii
anavyodhihirisha kwamba majanga hasa yanayodhuru afya na kusababisha kifo
yanavyoweza kumkengeusha binadamu kutokana na imani katika Mungu.
Katika sura ya nne, tumeangazia uchanganuzi-linganishi wa riwaya hizi mbili kuhusiana
na mikinzano ya mitazamo. Aidha, tumeangazia dhana ya Mungu katika riwaya hizi
mbili. Vile vile, tumeangalia kazi nyingine za fasihi ya Kiswahili ambazo
zimeshughulikia maswala ya udhanaishi na fumbo la Mungu.
Sura ya tano ni hitimisho na maelezo kuhusu mafanikio na matatizo pamoja na
mapendekezo. | en |