Show simple item record

dc.contributor.authorNyaosi, Kenneth N
dc.date.accessioned2013-05-03T11:57:29Z
dc.date.available2013-05-03T11:57:29Z
dc.date.issued2008
dc.identifier.citationMasters of artsen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/18688
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia matatizo yanayowakumba wanawake katika riwaya mbili za Kiswahili ambazo ni: Kiu ya Mohamed Suleiman na Msimu wa Vipepeo ya Kyallo Wamitila. Katika sura ya kwanza, tulionyesha tatizo la utafiti, sababu za kuchagua mada hii, upeo wa tasnifu, msingi wa nadharia na njia za utafiti. Katika utafiti huu, tumetumia tawi la nadharia ya ufeministi ambalo ni ufeministi asilia. Ufeministi asilia ni tawi linalosisitiza kuweko kwa usawa kati ya wanadamu wote bila kujali jinsia. Sura ya pili imeanza na uandishi wa Kyallo Wamitila pamoja na msimamo wake kuhusu asasi ya ndoa. Pia, tuliangalia aina mbalimbali za ndoa zinazotambuliwa kisheria nchini Kenya. Wakati huo huo tulishughulikia sababu mbali mbali zinazowafanya watu kufunga ndoa pamoja na sababu zilizowafanya wahusika kuoa au kuolewa katika Msimu wa Vipepeo na Kiu. Kwenye sura ya tatu, tulishughulikia tatizo letu la utafiti ambalo lilikuwa kuyajadili matatizo yanayowakumba wanawake katika ndoa kwa mujibu wa riwaya za Kiu na Msimu wa Vipepeo. Katika sehemu hii, tuligundua kwamba wanawake walio kwenye ndoa hupitia matatizo mbali mbali ambayo yanaendelezwa na waume zao pamoja na mfumo mzima wa jamii. Baadhi ya matatizo hayo ni: Uzinzi wa waume, ulevi na kutowajibika kwa wengi wa waume na umaskini kwenye asasi ya ndoa. Katika sura ya nne, tulishughulikia mikakati ambayo inaweza kuwekwa ili kupunguza matatizo ya mwanarnke katika ndoa. Baadhi ya mikakati ni pamoja na kuwa na muwasala kati ya rnke na mume, kuombana msamaha, kuwa na umoja na he shima kati yao. Katika sura ya tano tulishughulikia kwa kifupi matokeo ya utafiti wetu na kisha tukatoa mapendekezo kuhusu tafiti za baadaye.en
dc.description.sponsorshipUniversity of Nairobien
dc.language.isoenen
dc.titleTaswira ya asasi ya ndoa katika riwaya mbili za kiswahili: Kiu na Msimu wa vipepeoen
dc.typeThesisen


Files in this item

FilesSizeFormatView

There are no files associated with this item.

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record