Matatizo ya Leksikografia tafsiri: Tathmini ya Kamusi ya F. Johnson (1939)
View/ Open
Date
1996Author
Mwangi, Patrick I
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu yetu imejengwakatika msingi unaoafiki kuwa
kamusi za lugha mbilini kazi halisi za tafsiri. Tahakiki
nyingiambazo tayari zimeandikwa kuhusu matatizo ya
tafsiri zimeegemeazaidikatika fasihi na kazi za kidini. Sisi
tunaonyesha kuwa hata kamusi za lugha mbili zina matatizo
mengiya tafsiri katika ngazi mbalimbali za lugha. Tasnifu
yenyeweimegawanywakatika sura tano.
Katika sura ya kwanza, tumelifafanua somo letu la utaflti
ambalo ni leksikografia-tafsiri. Pia, tumeonyesha
madhumuni yetu katika utafiti huu na sababu zilizotufanya
tuchague somo hili. Fauka ya haya, tumeelezea upeo na
mipaka ya tasnifu yetu na pia yaleyaliyoandikwa kuhusu
somohili. Tumefafanua pia mwongozowa utafiti wetu na
nadharia tete. Mwisho,tumeeleza njia tutakazozitumia
katika utafiti wetu.
Katika sura ya pili,tumeifafanua dhana ya tafsiri huku
tukionyesha matatizo, umuhimu na nafasi yake. Aidha,
tumeifafanua dhana ya leksikografia ambapo tumeeleza
maana ya kamusi, mambo muhimu katika kamusi na aina
za kamusi. Hatimaye tumeifafanua dhana ya leksikografia-
tafsiri huku tukionyesha wale ambao hunufaisha na kamusi
zalugha mbili. Mwisho,tumeonyesha nafasi ya maana
katika tafsiri ya moja kwa moja, tafsiri-huru na tafsirimawasiliano.
Sura ya tatu inahusu mambo ya sarufl katika kamusi za
uwililugha. Tumeonyesha aina za sarufi, kisha
tumefafanua kuhusu matatizo ya kifonolojiakatika kamusi
zauwililugha na pia yaleya kimofolojiana kisintaksi.
Hatimaye, tumetoa mifanoya tafsiri zisizosahihi kimofolojia
na kisintaksi katika kamusi ya Johnson (1939)ya KingerezaKiswahiliambayo
tunaitathmini.
Sura ya nne ndiyo kiini c}?-akaziyetu. Tumeijadili ,dhana ya
semantiki, maana katika semantiki na pia matatizo ya
kisemantiki katika kamusi za uwililugha. Matatizo haya
yanahusu uchaguzi wavisawe, uchanganuzi wa maana,
maneno yajarnii rnojana ufafanuzi wa kimichoro na
kimifano. Hatimaye tumeyaonyesha matatizo hayo kama
yalivyojitokezakatika kamusi ya F.Johnson (1939).
Tumeonyesha pia makosa ya kisemantiki katika mifano
iliyotolewana mtunzi na matatizo mengineyajumla katika
kamusi hiyo.
Sura ya tano ni hitimisho. Tumeonyesha kwakifupiyaletuliyoyashughulikia,
yaliyojitokeza kuhusu nadharia-tete, ufaaji wa mwongozo wetu wa utafiti,
matatizo tuliyoyapata na kisha tunatoa mapendekezo yetu.
Citation
M.A (Swahili) 1996 ThesisSponsorhip
University of NairobiPublisher
Depatment of Linguistics, University of Nairobi
Description
Master of Arts Thesis