dc.description.abstract | Hii ni kazi ya kipekee iIiyozama sana katika utafiti wake na kutupeleka katika hali halisi isiyosomeka tu vitabuni bali katika dunia yetu ya leo. Kazi hii inachanganua taswira ya mwanamke kwa kurejelea tamthlia tatu za Wamitila, K. W ambazo ni Wingu La Kupita, (1999), Pango (2003) na Seserumbe (2009). Sura ya kwanza inashughulikia mapendekezo ya utafiti wetu ambapo nadharia ya Ufeministi wa Kiafrika imetumiwa iIi kuelezea masuala haya miongoni mwa mengine.
Sura ya pili inaanza kwa kutoa maelezo mafupi kumhusu Wamitila, K. W ambaye ndiye mwandishi wa tamthiIia tunazotafitia. Katika sura hii muhtasari wa tamthiIia ya Wingu La Kupita unatolewa kisha mifano ya wahusika wanawake inazungumziwa na maudhui mengine kubainishwa. Uchanganuzi wa kina kuhusu changamoto zinazomkumba mwanamke zimebainishwa hata taswira chanya na hasi ambayo mwanamke amepewa imetolewa. Pia mikakati anayoweza kuitumia iIi kuweza kujikomboa dhidi ya hali hizi imezungumziwa. Kila moja ya vipengele hivi katika tamthiIia ya Wingu La Kupita imelinganishwa na hali halisi katika jamii za Kiafrika kupitia baadhi ya kazi zilizoandikwa kumhusu mwanamke.
Sura ya tatu inachanganua tamthilia ya Pango. Muhtasari wa tamthilia hii unatolewa kwanza iIi kuwezesha uelewaji wake kisha msingi kuhusu wahusika wanawake na maudhui umeangaziwa kwa ufupi. Mifano mahsusi kutoka tamthilia ya Pango imetolewa kuridhia changamoto zinazomkumba mwanamke, taswira chanya na hasi ya mwanamke pamoja na njia anazoweza kuzitumia kukabiliana na changamoto mbalimbali maishani. Mifano hii katika tamthilia ya Pango imelinganishwa na hali halisi katika jamii za Kiafrika lakini ulinganishaji huu umepunguzwa katika sura hii ila kwa jambo jipya ambalo halikuangaziwa awali katika tamthilia ya Wingu La Kupita katika sura ya pili.
Sura ya nne inashughulikia tamthilia ya Seserumbe ambayo ndio ya kisasa zaidi kati ya ziIe za mwandishi huyu wakati tunapozifanyia utafiti. Vilevile sura hii inatoa muhtasari wa tamthiIia hii kisha maelezo kuhusu wahusika wanawake na maudhui mengine yanaangaziwa kwa ufupi. Njia ambazo zinadhihirisha mwanamke alivyodhalilishwa zimetolewa aidha jinsi alivyochorwa kwa njia chanya na hasi imebainishwa. Hatimaye mikakati ambayo mwanamke anachukua kuweza kujikomboa kutokana na changamoto mbalimbali imetolewa. Uchanganuzi wa vipengele hivi katika tamthilia ya Seserumbe umelinganishwa na matukio halisi katika jamii kwa yale masuala mapya zaidi na ambayo hayakuangaziwa katika tamthilia za awali Wingu La Kupita na Pango.
Tanahitimisha utafiti wetu katika sura ya tano ambapo tunalinganisha na kutofautisha matatizo yanayomkabili mwanamke, taswira chanya na hasi, na ukombozi wake katika tamthilia za Wlngu La Kupita, Pango na Seserumbe. Mtazamo wa mwandishi na wa utafiti huu kuhusu jinsi mwanamke alivyochorwa kijumla katika kila moja ya tamthilia hizi umetolewa. Mambo kuhusu utumiaji wa majina, idadi, majukumu na kukuzwa kwa mwanamke yamebainishwa. Hatimaye maswali yakijumla kumhusu mwanamke yametajwa na mapendekezo kuhusu utafiti wa baadaye kutolewa. | en_US |