Ukiushi wa viambishi-vipatanishi unaojitokeza katika kazi za Kiswahili zilizoandikwa na wanafunzi wa shule za Upili jijini Nairobi
Abstract
Tasnifu hii inashughulikia ukiushi wa viambishi-vipatanishi vya ngeli za 3, 4, 6, 9, 10, 11 na 14 unaotokea katika shule za upili za jijini Nairobi. Utafiti huu umezingatia mtazamo wa uchanganuzi wa upotofu. Timeigawa kazi hii katika sura nne. Katika sura ya kwanza nimezungurnzia yafuatayo: utangulizi kuhusu mada inayoshughulikiwa, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti,· nadharia tete, umuhimu wa kushughulikia tatizo hili, upeo na mipaka, yaliyoandikiwa kuhusu uchaganuzi upotofu, msingi wa nadharia, njia za utafiti, ukusanyaji wa data na uchanganuzi wake.
Sura ya pili inahusu uainishaji wa ngeli za Kiswahili sanifu. Sura hii inatoa maelezo kuhusu suala muhimu la ngeli za Kiswahili sanifu na kuonyesha jinsi mbali mbali zilizoturniwa kuainishia ngeli za Kiswahili sanifu. Sura ya tatu inahusu uchanganuzi wa data na sababu za upotofu. Makosa haya yameainishwa katika kategoria tofauti na maelelzo kutolewa kuhusiana na sababu zilizopelekea makosa yenyewe kutokea.
Katika sura hii ndipo viambishi- vipatanishi vilivyokiukwa zaidi vilibainika baada ya uchanganuzi wa data. Mwisho ni sura ya nne, ambayo inahusu· hitimisho la kazi nzima na mapendekezo kwa upotofu uIiojitokeza. Surahii Imebeba mapendekezo mbalimbali yatakayowafaa watafiti wengine wa siku za usoni.
Publisher
University of Nairobi, Kenya