dc.description.abstract | Katika tasnifu hii iliyolenga kuzipambanua sifa za kishujaa za Furno Liyongo na Lwanda
Magere pamoja na umuhimu wao kwajamii zao, imekuwa najumla ya faslu tano. Katika kila
faslu tumeshughulikia masuala na vipengele fulani maalum ambavyo vinaingiliana na
kukamilishana.
Katika faslu ya kwanza tumeangazia usuli wa tasnifu. Tumetanguliza kwa kutoa fasiri kuhusu
dhana ya mashujaa na kutoa mifano ya baadhi ya shujaa duniani. Aidha, tumegusia kijuujuu
masuala ya jamii na taasisi ya kishujaa. Tumefafanua somo la utafiti, maswali ya utafiti,
madhumuni ya utafiti pamoja na nadharia tete. Pia, tumeeleza sababu za kulichagua somo
pamoja na kufafanua nadharia ambazo zitatuongoza katika mchakato mzima wa utafiti wetu
na njia za utafiti ambazo tutazitumia kupata data ili kutekeleza madhumuni ya utafiti wetu.
Katika faslu ya pili, tumefafanua historia ya Furno Liyongo na Lwanda Magere kwa
kuifungamanisha na historia ya jamii zao, Waswahili.na jamii' ya Wajaluo mtawalia. Kwa
-; ;
sababu majagina hawazuki katika li{~we tupu, tumetoa taswira ya mazingira, yaani
mazingira ya kitamaduni (ya kijamii, kisiasa na kiuchumi), hali ya kijamii na kipindi
ambacho Lwanda Magere na Furno Liyongo walizuka. Aidha, tumeeleza masuala muhimu
katika maisha yao.
f
Katika faslu ya tatu tumelenga kuzilinganisha sifa za kishujaa za Lwanda Magere na Furno
Liyongo. Tumezipambanua sifa hizi kW<1kina huku tukionyesha kiwango cha kufanana na
kutofautiana kwa sifa hizi.
Katika faslu ya nne tumejikita katika ufafanuzi wa umuhimu wa Furno Liyongo na Lwanda
Magere kwa jamii zao. Ni katika faslu hii ambapo tumerejelea "taasisi ya shujaa" kama
mojawapo ya taasisi nyingi katika mfumo wa jamii yoyote ile na taasisi ambayo huzuka ili
",
kutekeleza mahitaji fulani katika jamii. Katika harakati za mashujaa kutimiza mahitaji haya,
ndipo umuhimu wao umedhihirika.
Katika faslu ya tano tumejumlisha hitimisho ya tasnifu na mapendekezo kuhusu utafiti wa
ziada na wa baadaye. Tumeangazia masuala ya kijumla na haswa yanayohusu matokeo ya
utafiti wetu. Aidha, tumependekeza baadhi ya masuala ambayo watafiti wa baadaye
wataweza kuyamulika. | en |