Ulinganishi Wa Matumizi Ya Tasfida Za Muktadha Wa Nyumbani Katika Lugha Ya Kikamba Na Kiswahili
Abstract
Tasnifu hii imeshughulika na kulinganisha matumizi ya tasfida katika lugha ya Kikamba
na ya Kiswahili. Ingawa tasnifu hii imetolewa kwa mahitaji ya shahada ya Kiswahili,
data iliyochanganuliwa ni kutoka lugha ya Kikamba na ya Kiswahili. Uchanguzi huu
tuliufikia kwa kutambua umuhimu unaostahili kupewa lugha zetu nyingine za Kiafrika
katika muktadha wa nyumbani na miktadha mingine mbalimbali.
Kwa sababu ya juhudi zinazofanywa na kila jamii kuikuza na kustawisha maadili katika
maisha ya binadamu wote (Stockwell, 2008). Ndiposa tukawa na jukumu la kuchunguza
matumizi ya tasfida za nyumbani. Somo la tasnifu hii ni ulinganishi wa matumizi ya
tasfida katika lugha ya Kikamba na Kiswahili katika muktadha wa nyumbani.
Tumechunguza matumizi ya tasfida kwa lugha ya Kikamba na kulinganisha na matumizi
katika lugha ya Kiswahili. Hatukulinganisha matumizi ya tasfida katika lugha hizi mbili
kwa kutaka kulingamisha tu bali, kwa kufanya hivyo tumetoa mwanga zaidi kuonyesha
kuwa, tasfida ni chombo muhimu na maalum cha mawasiliano katika jamii yoyote.
Tumeonyesha kwamba jamii mbili zinazotofautiana kwa mengi huweza kuwa na mawazo
sawa kuhusu jamii na mazingira yao kwa jumla.
Madhumuni makuu katika tasnifu hii yalikuwa kulinganisha matumizi ya tasfida katika
lugha hizi mbili, Kikamba na Kiswahili ili kudhibitisha kuwa, kunao uhusiano mkubwa
katika matumizi ya tasfida. Tumechambua jinsi matumizi ya tasfida hufanikisha
mawasiliano katika lugha ya Kikamba na Kiswahili. Tulikuwa na shabaha pia ya
kuchunguza jinsi hali za jamii kama umri, Kazi, jinsias na hadhi huathini matumizi ya
tasfida.
vii
Data ilikusanywa kupitia mahojiano na hojaji zilijazwa na watafitiwa wateule. Data
iliyokusanywa ilichanganuliwa na kubainishwa kwa msingi wa nadharia ya Upole
iliyoasisiwa na Penelope Brown na Levinson (1978).
Citation
Tasnifu hii imetolewa ili kutosheleza baadhi ya mahitaji ya shahada ya uzamili katika Chuo Kikuu cha NairobiPublisher
University of Nairobi