Show simple item record

dc.contributor.authorNyandago, Francis O
dc.date.accessioned2013-11-26T11:57:06Z
dc.date.available2013-11-26T11:57:06Z
dc.date.issued2013
dc.identifier.citationMaster of Artsen
dc.identifier.urihttp://erepository.uonbi.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/60461
dc.description.abstractLengo la tasnifu hii ni kufanya uchunguzi linganishi wa sentensi sharti ya Kiswahili Sanifu na Ekegusii kwa kutumia nadharia ya Upanuzi wa Sarufi Sawazishi. Tumeigawa kazi hii katika sura tano. Katika sura ya kwanza, tumetoa maelezo ya kimsingi yanayohusu somo la utafiti, madhumuni ya utafiti na upeo wa tasnifu. Masuala mengine ambayo yameshughulikiwa ni pamoja na sababu za kulichagua somo, nadharia tete, yaliyoandikwa kuhusu somo hili, msingi wa nadharia na mbinu za utafiti. Sura ya pili inalenga kushughulikia sintaksia ya sentensi sharti ya Kiswahili Sanifu. Sura imeanza kwa kutoa fasili ya sentensi sharti ya Kiswahili na ufafanuzi wa viambajengo vyake. Viambajengo hivi ni pamoja na kishazi sharti, kishazi shurutiwa, vitambulishi sharti na viunganishi viambatishi. Vipashio vinavyotumiwa kutolea masharti vimetambuliwa na kufafanuliwa. Vipashio hivi ni pamoja na ‘kama, ikiwa, endapo, iwapo, ki, nga, ngali, nge na ngeli’. Suala lingine lililoshughulikiwa katika sura hili ni muundo wa sentensi sharti ya Kiswahili na ugeuzi unaojitokeza katika kuigeuza sentensi sharti kutoka kiwango cha muundo msingi hadi kile cha muundo geuzi. Imebainishwa kuwa sentensi sharti ya Kiswahili ikiwa katika kiwango cha muundo msingi huwa na kishazi shurutiwa mwanzoni kikifuatwa na kishazi sharti. Vishazi hivi huunganishwa kwa mujibu wa kitambulishi sharti kinachokitegemeza kishazi sharti kwa kishazi shurutiwa. Sentensi hiyo inapogeuzwa hadi kiwango cha muundo geuzi, kanuni ya ugeuzi hukitanguliza kishazi sharti kikifuatwa na kishazi shurutiwa. Wakati wa ugeuzi huo, kiunganishi kiambatishi kisicho cha lazima hutokea na kukitegemeza kishazi sharti kwa kishazi shurutiwa. Sura ya tatu inashughulikia fasili ya sentensi sharti ya Ekegusii na ufafanuzi wa viambajengo vyake. Viambajengo hivi ni pamoja na kishazi sharti, kishazi shurutiwa, vitambulishi sharti na viunganishi viambatishi. Imebainika kuwa sentensi sharti ya Ekegusii huundwa kwa kishazi sharti na kishazi shurutiwa. Vitambulishi sharti katika lugha ya Ekegusii ni pamoja na ‘onye, -ise, -are, k- na ebe’. Kuna kiunganishi kiambatishi kitumiwacho ambacho si cha lazima kinachotumiwa kukiunganisha kishazi sharti na kishazi shurutiwa. Kiunganishi hiki ni ‘rirorio’ ambacho hudhihirika katika kiwango cha muundo geuzi pekee. Mengine yaliyoshughulikiwa katika sura hii ni muundo wa sentensi sharti ya Ekegusii na ugeuzi unaojitokeza katika kuigeuza sentensi sharti kutoka kiwango cha muundo msingi hadi kile cha muundo geuzi. Uchunguzi umepata kuwa sentensi sharti ya Ekegusii ikiwa katika kiwango cha muundo msingi huwa na kishazi shurutiwa kikitangulia mwanzoni mwa sentensi kikifuatwa na kishazi shurutiwa. Kishazi sharti hutegemezwa kwa kishazi shurutiwa kwa matumizi ya kitambulishi sharti kinachotekeleza pia jukumu la kutambulisha sharti. Sentensi sharti hugeuzwa kutoka kiwango cha muundo msingi hadi muundo geuzi kutokana na ugeuzi unaokitanguliza kishazi sharti kikifuatwa na kishazi shurutiwa. Ugeuzi huo husababisha kutokea kwa kiunganishi kiambatishi ‘rirorio’ kisicho cha lazima na kinachoviunganisha vishazi husika kwa kukitegemeza kishazi sharti kwa kishazi shurutiwa. Katika sura ya nne, ulinganishi wa vipengele mbali mbali vinavyohusiana na sintaksia ya sentensi sharti ya Kiswahili sanifu na Ekegusii umefanywa. Kumeshughulikiwa uainishaji wa sentensi sharti ya Kiswahili na Ekegusii, kufanana na kutofautiana kwa kishazi sharti cha Kiswahili na cha Ekegusii, kufanana na kutofautiana kwa miundo ya sentensi sharti ya Kiswahili na Ekegusii na ulinganishi wa michakato ya ugeuzi inayogeuza sentensi sharti kutoka kiwango cha muundo msingi hadi kile cha muundo geuzi. Sura ya tano inatoa mahitimisho ya kijumla ya tasnifu hii. Inaanganzia masuala muhimu yaliyoshughulikiwa na mahitimisho yao katika kila sura ya tasnifu hii na kisha kutoa mapendekezo kulingana na maoni ya mtafiti.en
dc.language.isoenen
dc.publisherUniversity of Nairobien
dc.titleUchanganuzi Linganishi Wa Sintaksia Ya Sentensi Sharti Ya Kiswahili Sanifu Na Ekegusiien
dc.typeThesisen
local.publisherDepartment of literature and languageen


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record