Show simple item record

dc.contributor.authorSabula, Millicent A
dc.date.accessioned2014-12-01T08:35:44Z
dc.date.available2014-12-01T08:35:44Z
dc.date.issued2014
dc.identifier.citationMaster of Arts in Kiswahilien_US
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/75733
dc.description.abstractFasihi ya kiekolojia ni uwanja uliochipuka miaka ya 1970 na kuendelea miaka ya 1990 kuchanganua, kuchambua na kuhakiki kazi za kifasihi. Uwanja huu unalenga kuangazia fani na maudhui katika matawi ya fasihi kiekolojia kama vile ya Kiafrika, Kimarekani na Kifeministi. Utafiti huu unahusu nafasi ya wanawake katika uhifadhi wa mazingira kwa mtazamo wa fasihi ya ufeministi wa kiekolojia. Lengo kuu la utafiti huu ni kupambanua mchango wa ufeministi wa kiekolojia katika fasihi ya Kiswahili. Utafiti huu uliongozwa na madhumuni haya: kubainisha mchango wa ufeministi wa kiekolojia katika uhifadhi wa mazingira katika riwaya ya Nakuruto; kupambanua mhusika Nakuruto na mchango anaoutoa katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira; kujadili kwa kina changamoto anazopitia mwanawake katika kuhifadhi mazingira; kujadili athari za masuala ya kimazingira na jinsi zinavyojitokeza katika riwaya. Nadharia iliyotumika katika utafiti huu ni nadharia ya Ufeministi wa kiekolojia iliyoasisiwa na mfaransa Francoise d‘Eaubonne mwaka wa 1974. Nadharia hii ilibuniwa kwa ajili ya kuleta mapinduzi ya kiekolojia hasa kwa kumzingatia mwanamke. Utafiti huu ulifuata muundo wa uchanganuzi wa makala ambapo maelezo yetu yaliangazia masuala tata yaliyoko kwenye matini tuele. Makala ya kimsingi ya utafiti yalikuwa ni riwaya ya Nakuruto ilhali makala ya sekondari yalitokana na usomaji wa vitabu na makala yaliyohusu mada. Utafiti huu ulibainisha kwamba ufeministi wa kiekolojia una nafasi ya kuwazindua wanawake ili kuleta ukombozi wa kimazingira. Aidha, utafiti ulitambua kuwa mhusika Nakuruto aliwazindua wanajamii kupitia kwa elimu na maarifa yake ya kimazingira, hivyo kusababisha mapinduzi. Utafiti ulitambua kwamba wanawake wanasimangwa, kutukanwa, kudharauliwa na kudunishwa wanapojihusisha na harakati za utunzaji mazingira. Mwisho utafiti ulitambua kwamba umaskini, kukauka kwa chemichemi za maji, uskwota, magonjwa na vifo ni athari zinazosababishwa na uharibu wa mazingira. Utafiti huu ulihitimisha kwamba mwanamke anastahili kupewa nafasi katika uhifadhi wa mazingira na kwamba, fasihi ya Kiswahili ina uwezo wa kumulika masuala ya kielokojia kama yanavyojitokeza katika jamii. Kwa kuwa utafiti huu haukuweza kuchunguza vipengele vyote vya kifasihi mazingira, mtafiti anapendekeza kwamba utafiti wa baadaye uzingatie mikabala mingine kama vile fasihi mazingira kieneo, Kiafrika na Kimagharibi, hasa kwa mkondo wa kilinganishien_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleNafasi ya wanawake katika uhifadhi wa mazingira katika riwaya ya Nakuruto : mtazamo wa fasihi ya ufeministi wa kiekolojiaen_US
dc.typeThesisen_US
dc.type.materialen_USen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record