dc.description.abstract | Huu utafiti ulihusu matumizi ya nadharia ya vitendo usemi kusuluhisha tatizo la ulinganifu
katika tafsiri. Msisitizo ulitiliwa kwenye ngazi ya ilokusheni ambapo swali kuu lililoongoza
utafiti wenyewe ni kutatokea nini iwapo nadharia ya vitendo usemi (VU) itahuruhijwa na
kutumiwa kama msingi wa kushughulikia tafsiri ya Kiswahili? Nadharia ya VU inaweza kuwa
faafu, iwapo, mihimili yake itaeleweka na jinsi VU huibuliwa katika lugha lengwa (LL). Miundo
ya kuibua VU ambavyo tumeainisha kwa kuzingatia kielelezo cha Searle imeshughulikiwa.
Nadharia za ulinganifu na ufasiri zimetumiwa kwenye uchunguzi huu. Ili kutathmini ufaafu wa
nadharia yenyewe katika kusuluhisha matatizo ya utafiti, nadharia za ufasiri na ulinganifu
zimetumiwa kuchunguza tafsiri za kazi mbili za Barbara Kimenye zilizoteuliwa kama kielelezo
huku ukamilifu wa lugha katika mikabala ya isimu, fasihi na ishara ukizingatiwa. Mifano ya VU
mbalimbali vinavyojitokeza kwenye kazi hizi imechanganuliwa. Pale kunakojitokeza
usolinganifu, tunapendekeza tafsiri faafu kwa mujibu wa isimu tendaji. Tumesisitiza umuhimu
wa kuzingatia vipengele vya pragmatiki katika uibushi wa maana ili kufanikisha mawasiliano. | en_US |