Show simple item record

dc.contributor.authorMakange, Joseph L
dc.date.accessioned2015-12-11T12:36:32Z
dc.date.available2015-12-11T12:36:32Z
dc.date.issued2015
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/93440
dc.descriptionThesisen_US
dc.description.abstractNafasi ya fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Waswahili na Wataveta ni utafiti wenye gharadhi ya kuonyesha jinsi fani za kiutendi zinavyotumiwa katika nyimbo zinazoimbwa wakati wa harusi.Tulichokusudia kufanya katika utafiti wetu ni kulinganisha fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Wataveta na ile ya Waswahili.Malengo ambayo tulikusudia kuangazia ni kubainisha aina mbali mbali za fani za kiutendi,kuonyesha umuhimu wa fani za kiutendi, kubainisha kuwepo au kutokuwepo kwa fani za kiutendi katika nyimbo za harusi na kuonyesha nyimbo mbalimbali zinazoimbwa katika sherehe za harusi miongoni mwa jamii ya Waswahili na Wataveta.Dira iliyotuongoza kuangazia mada yetu ni nadharia ya Sosholojia ya Utendaji iliyoasisiwa na Bronislaw Malinowski kutoka Uholanzi na Radcliffe-Brown kutoka Uingereza.Vile vile tulitumia mtazamo wa viziada lugha wa Okpewho (1992) katika kuelezea fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Waswahili na Wataveta.Katika utafiti wetu tuliongozwa na nadharia tete mbili.Kwanza, tulitaka kubainisha ya kwamba fani za kiutendi ni za aina mbalimbali katika jamii ya Wataveta na ile ya Waswahili.Pili, tulitaka kudhibitisha ya kwamba fani za kiutendi katika nyimbo za harusi zina uhusiano miongoni mwa jamii ya Wataveta na ile ya Waswahili.Mbinu ya utafiti iliyotumiwa ni ile ya sampuli lengwa.Tuliweza kutembelea maktabani na kusoma baadhi ya tasnifu zilizoandikwa.Ushauri wa wahadhiri wetu ulitufaa sana kwani ulikuwa mhimili mkuu wa kazi hii.Utafiti wetu ulimalizikia nyanjani ambapo tuliwahoji watu kumi wenye umri kati ya miaka thelathini hadi themanini(30-80) kutoka katika jamii ya Wataveta na ile ya Waswahili.Tulihudhuria harusi tatu kutoka katika jamii hizi na tukachagua nyimbo tano (5) kutoka kila jamii.Utafiti huu umedhihirisha kuwepo kwa uhusiano katika fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii hizi mbili kama vile: minenguo ya mwili,kiitikio,kunyamaza kimya na ishara za uso.Utafiti huu pia umebaini ya kuwa kuna fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii hizi mbili ambazo hazina uhusiano, kama vile: maleba na matumizi ya vidole na mikonoen_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleUlinganishaji wa fani za kiutendi katika nyimbo za harusi miongoni mwa jamii ya Wataveta na Waswahilien_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record