dc.description.abstract | Madhumuni ya utafiti huu yalikuwa kuchunguza uwasilishwaji wa wahusika wa kike
kimajukumu katika Mbali na Nyumbani kwa lengo la kubainisha kuwepo na “kutokuwepo”
kwao kwa uwazi katika baadhi ya miktadha na “kutokuwepo” kwao kwa uwazi katika miktadha
mingine. Ubainishaji huu ulilenga kuonyesha sababu nzuri na chanya za kihistoria na
kianthropolojia ambazo zinaeleza uwasilishwaji wa aina hiyo.
Tulidurusu kazi mbali mbali ambazo zimechunguza masuala ya usawiri na taswira ya wanawake
ili tufahamu jinsi tathmini zimehitishwa. Nadharia iliyoongoza utafiti huu ni tapo la
anthropolojia ambalo ni anthropolojia ya kiutamaduni na kijamii. Nadharia hii inatambua
kuchunguzwa kwa masuala ya wanawake kihistoria, uhalisi wa maisha katika jamii na michakato
ya kianthropolojia ili kuwapa wanawake tathmini chanya.
Matokeo ya utafiti yalidhihirisha kwamba, sababu za kuwepo na “kutokuwepo” kwa wahusika
wa kike katika mazingira na miktadha katika Mbali na Nyumbani ni za kihistoria na
kianthropolojia bali sio za kiusawiri. Utafiti ulionyesha pia kwamba, baadhi ya tathmini hasi
katika tafiti za awali zinaweza kufikiriwa upya. | en_US |