Show simple item record

dc.contributor.authorGathara, Francisco K
dc.date.accessioned2016-04-22T12:21:41Z
dc.date.available2016-04-22T12:21:41Z
dc.date.issued2015-11
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/94927
dc.description.abstractUtafiti huu ulikusudia kufafanua taswira ya jagina katika utendi, kwa kumrejelea shujaa Fumo Liyongo kama alivyoelezwa katika Utenzi wa Fumo Liyongo wake Muhammed Kijumwa (1913), na Nabii Isa kama alivyoelezwa katika Utenzi wa Nabii Isa, wake Musa Mshenga (1977). Madhumuni makuu katika utafiti huu yalikuwa ni kulinganisha na kutofautisha sifa za kijagina za Nabii Isa na Fumo Liyongo, kwa nia ya kudhibitisha kuwa, sira za majagina kutoka jamii mbili zinazotofautiana katika mazingira, mila na desturi, zinaweza kufanana sana. Uchanguzi huu tuliufikia baada ya kutambua kuwa majagina wa kidini na wa kihistoria hawajatafitiwa kikamilifu. Tumeangalia historia na maisha ya Fumo Liyongo na Nabii Isa, pamoja na historia ya jamii zilizowazaa na kuwakuza, kisha tukalinganisha na kutofautisha sifa zao za kijagina kwa mujibu wa sifa bia za mashujaa. Aidha, tumeangazia umuhimu wa mashujaa hawa kwa jamii zao. Data ilikusanywa maktabani na mtandaoni, kuchanganuliwa na kubainishwa kwa msingi wa nadharia ya Uhakiki wa Vikale iliyoasisiwa na Carl Jung. Matokeo ya utafiti huu yalilingana na nadharia tete zilizoongoza mchakato mzima wa utafiti huu. Ilidhihirika kuwa Liyongo na Nabii Isa ni mifano mizuri ya jagina wa kihistoria na wa kidini. Mashujaa hawa pia wametokea kuwa muhimu sana katika historia ya jamii zao, na kwa ulimwengu mzima kwa jumla, na kuwa wanaweza kuwekwa katika viwango sawa na mashujaa wengine ulimwenguni. Matokeo haya vilevile yalidhihirisha kuwa, sifa za mashujaa hawa kwa kiasi kikubwa zinafanana.en_US
dc.language.isoenen_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.titleTaswira ya jagina katika tendi: ulinganishi wa fumo liyongo na nabii isaen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record