Uhakiki Wa Mtindo Katika Vipanya Vya Maabara
View/ Open
Date
2014-10Author
Tsuma, Samuel M
Type
ThesisLanguage
otherMetadata
Show full item recordAbstract
Tasnifu hii imeshughulikia uhakiki wa mtindo katika Vipanya vya Maabara. Tumetumia
nadharia ya umuundo kwa kuwa, nadharia hii hubainisha vipengele vya kimtindo
ambavyo ni tashihisi, maswali ya balagha, italiki na vinginevyo. Kufaulu kwa kazi ya
kifasihi, hutokana na mbinu za kimtindo ambazo msanii amezitumia. Tumechanganua
vipengele vya kimtindo katika riwaya teule. Vipengele hivi ni sintaksia, italiki, tamathali
za semi na uwasilishaji wa mawazo. Tumegundua kuwa msanii amevitumia vipengele
vya kimtindo kwa njia nzuri kupitisha ujumbe wake kwa hadhira.
Kazi imegawika katika sura nne. Katika sura ya kwanza, tumeshughulikia maswala ya
kimsingi yanayojenga utafiti kama vile: utangulizi kuhusu mada, sababu za kuchagua
somo, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, msingi wa kinadharia, njia za
utafiti, upeo na mipaka.
Katika sura ya pili, tumeshughulikia riwaya na uchanganuzi wa kimtindo. Tumeeleza
maana ya riwaya kuwa ni hadithi ndefu iliyobuniwa na kuandikwa kwa nathari. Riwaya
ni sharti iwe na migogoro, wahusika ambao ni binadamu au wanyama wachukuwao
sifa za binadamu. Pia tumeeleza mtindo kuwa ni mtu, ni tabia, ni lugha na ni maisha
kutegemea mawazo ya mtu binafsi.
Katika sura ya tatu, tumehakiki mtindo wa Vipanya vva Maabara kwa kuchanganua hasa
vipengele vya kimtindo. Tumeona kuwa mwandishi amefaulu kutumia vipengele vya
kimtindo na kubainisha dhamira ya kazi yake. Ameweza kupitisha ujumbe wake vizuri
kwa msomaji.
Katika sura ya nne, tumetoa mahitimisho, upimaji wa nadharia tete na mapendekezo.
Tumeona kuwa nadharia tete zote tatu zimetimizwa. Vipengele vya kimtindo vimetumika
sawasawa katika riwaya teule. Mfano kuna uzungumzinafsia na dayalojia baina ya
wahusika, tashbihi, tashihisi na nyinginezo. Msanii amefaulu kuptisha ujumbe kwa mnato
kutokana na mtindo aliotumia. Ametumia maswali ya balagha, italiki, uzungumzi wa
ainaaina na matumizi ya sentensi zisizokamilishwa. Tumependekeza wasomi wengine
kutafiti juu ya vipengele vya kidhamira, maudhui na mengine.
Publisher
University of Nairobi