Show simple item record

dc.contributor.authorTsuma, Samuel M
dc.date.accessioned2016-05-01T12:23:59Z
dc.date.available2016-05-01T12:23:59Z
dc.date.issued2014-10
dc.identifier.urihttp://hdl.handle.net/11295/95405
dc.description.abstractTasnifu hii imeshughulikia uhakiki wa mtindo katika Vipanya vya Maabara. Tumetumia nadharia ya umuundo kwa kuwa, nadharia hii hubainisha vipengele vya kimtindo ambavyo ni tashihisi, maswali ya balagha, italiki na vinginevyo. Kufaulu kwa kazi ya kifasihi, hutokana na mbinu za kimtindo ambazo msanii amezitumia. Tumechanganua vipengele vya kimtindo katika riwaya teule. Vipengele hivi ni sintaksia, italiki, tamathali za semi na uwasilishaji wa mawazo. Tumegundua kuwa msanii amevitumia vipengele vya kimtindo kwa njia nzuri kupitisha ujumbe wake kwa hadhira. Kazi imegawika katika sura nne. Katika sura ya kwanza, tumeshughulikia maswala ya kimsingi yanayojenga utafiti kama vile: utangulizi kuhusu mada, sababu za kuchagua somo, tatizo la utafiti, madhumuni ya utafiti, nadharia tete, msingi wa kinadharia, njia za utafiti, upeo na mipaka. Katika sura ya pili, tumeshughulikia riwaya na uchanganuzi wa kimtindo. Tumeeleza maana ya riwaya kuwa ni hadithi ndefu iliyobuniwa na kuandikwa kwa nathari. Riwaya ni sharti iwe na migogoro, wahusika ambao ni binadamu au wanyama wachukuwao sifa za binadamu. Pia tumeeleza mtindo kuwa ni mtu, ni tabia, ni lugha na ni maisha kutegemea mawazo ya mtu binafsi. Katika sura ya tatu, tumehakiki mtindo wa Vipanya vva Maabara kwa kuchanganua hasa vipengele vya kimtindo. Tumeona kuwa mwandishi amefaulu kutumia vipengele vya kimtindo na kubainisha dhamira ya kazi yake. Ameweza kupitisha ujumbe wake vizuri kwa msomaji. Katika sura ya nne, tumetoa mahitimisho, upimaji wa nadharia tete na mapendekezo. Tumeona kuwa nadharia tete zote tatu zimetimizwa. Vipengele vya kimtindo vimetumika sawasawa katika riwaya teule. Mfano kuna uzungumzinafsia na dayalojia baina ya wahusika, tashbihi, tashihisi na nyinginezo. Msanii amefaulu kuptisha ujumbe kwa mnato kutokana na mtindo aliotumia. Ametumia maswali ya balagha, italiki, uzungumzi wa ainaaina na matumizi ya sentensi zisizokamilishwa. Tumependekeza wasomi wengine kutafiti juu ya vipengele vya kidhamira, maudhui na mengine.en_US
dc.language.isootheren_US
dc.publisherUniversity of Nairobien_US
dc.subjectUhakiki Wa Mtindo Katika Vipanya Vya Maabaraen_US
dc.titleUhakiki Wa Mtindo Katika Vipanya Vya Maabaraen_US
dc.typeThesisen_US


Files in this item

Thumbnail

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record